Aneny Nahum Wakili wa kujitegemea akiwasilisha mada kuhusu Haki na uhusiano wa wafanyakazi mahala pa kazi ambayo ni Shera namba 6 ya mwaka 2004 sura namba 366 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini. Semina hiyo inaendelea kwenye hoteli ya Coral Beach Masaki Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam jana Jumamosi 13, 2021, Semina hiyo iliandaliwa na Shirika lilisilokuwa la Kiserikali la ActionAid.
Amney Manangwa Meneja Miradi ya Wanawake shirika la ActionAid akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika semina kuhusu Haki na uhusiano wa wafanyakazi mahala pa kazi ambayo ni Shera namba 6 ya mwaka 2004 sura namba 366 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Bi. Fransisca Camilius Clement Mratibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi,Mahoteli, Majumbani na Kazi Nyinginezo Zanzibar CHODAWU- Z akiwasilisha mada wakati semina hiyo ikiendelea kulia ni Emmanuel Mabodo Afisa Mradi Shirika la ActionAid.
Picha Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia wakati mada zilipokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la ActionAid limetoa mafuzo kwa waandishi wa habari vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini juu ya Mkataba wa Kimataifa wa shirika la kazi duniani unaolenga kupinga Ukatili wa kijinsia mahali pa kazi.
Mkataba huo unaojulikana kama ILO Convention C-190 on Violence and Harrassment una vifungu vyote vinavyoweza kusaidia kupunguza, kuondoa unyanyasaji na ukatili mahala pakazi.
Akitoa mada wakati wa mafunzo hayo Wakili, Anneny Nahum alivitaja baadhi ya viashiria vya unyanyasaji na ukatili mahala pa kazi ni pamoja na Unyanyasaji wa kimwili, Unyanyasaji kijinsia, Kiuchumi pamoja na kingono ambavyo mtu anaweza kufanyiwa na muajili, mfanyakazi au mwenzie.
Hata hivyo Nahum amesema kuwa vitendo vyote hivyo vinaweza kuondolewa ama kupunguzwa kama jamii kwa ujumla ikiwa na uelewa wa moja kwa moja kupitia serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kusaini makubaliano ya Mkataba huo ili uweze kutumika hapa nchini ingawa kuna baadhi ya vifungu vya sheria vipo katika katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Amesema mchakato wa Kuridhia Mkataba wa C-190 utasaidia sana maendeleo ya nchi pamoja na Mfanyakazi mmoja mmoja hasa katika kipengele cha Uchumi kwani kila mtu ambaye ni mfanyakazi wa sekta binafsi na serikali kila mmoja atapata haki yake pasi na kunyanyaswa wala kufanyiwa ukatili wowote kwani katika mkataba huo unatafsiri ni nani mfanyakazi.
Kwa Upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Action Aid, Amney Manangwa amesema kuwa lengo kubwa la mkataba huo ni Usalama na ulinzi Mahala pa kazi na kuona Tanzania yenye haki na Usawa.
“Sio mwajili aangalie nani wa kumpa ajira kuwa huyu ni Mlemavu, mweusi, mweupe, mwanamke, Mwanaume, wote wana haki ya kupata kazi huku kigezo kikubwa cha kupata ajira kiwe ni elimu ya mtu na uzoefu.” Amesema Amney
Amesema kuwa Mifumo ya Sheria na sera za nchi zizingatie zaidi katika kujua mikataba mbalimbali ya kimataifa iliyoweza kusaidia Wanawake, watoto, watu wenye ulemavu kupata haki sawa na watu wengine katika jamii.
Licha ya hayo Mratibu wa Chama cha Wafanyakazi wa hifadhi, mahotelini, Majumbani na kazi nyinginezo Zanzibar (CHODAWU-Z), Fransica Clement amesema kwa upande wa Zanzibar imeshakubali kujengwa kwa mahakama ya kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia. Ambayo itakuwa na shughuli hiyo tuu kwani Zanzibar matukio yanayoripotiwa ni macheche kuliko ambayo hayaripotiwi.
Ameongeza kuwa Mahakama hiyo itakapokuwa tayari wananchi kwa ujumla watakuwa na mahala pa kupeleka kesi zao za unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kiuchumi, Kimwili pamoja na Kisaikolojia ili wanaotenda makosa hayo waweze kuwajibishwa.
Fransisca ameiomba serikali kuridhia Mkataba huu wa Kimataifa wa shirika la kazi duniani wa C-190 uliotolewa kwa ajili ya kuondoa ukatili wa kijinsia katika maeneo ya kazi, hata hivyo suala la ukatili wa kijinsia liwe la kitaifa ili jamiii kwa ujumla iweze kuondokana na Changamoto hii ili taifa la Tanzania liwe sawa mahala pa kazi.