Home Mchanganyiko WATAKIWA KUCHAGUA TAALUMA ZITAKAZO WASAIDIA KUJIAJIRI

WATAKIWA KUCHAGUA TAALUMA ZITAKAZO WASAIDIA KUJIAJIRI

0

Mkufunzi wa chuo kikuu Cha Nelson Mandela kilichopo mkoani hapa Prof. Verdiana Grace Masanja wa kwanza kulia akipokea picha iliochorwa na mwanafunzi wa kidato Cha nne wa shule ya sekondari ya Edmond rice Mussa Michael  juzi alipokuwa mgeni rasmi Katika mahafali ya kidato Cha sita shuleni hapo wa kwanza kulia mkuu wa shule hiyo Simon Kaswahili pamoja na   mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari  Edmond rice,ambaye pia ni mkufunzi wa chuo kikuu Cha SAUT wakili Emanuel Sood (picha na Woinde Shizza , ARUSHA).

*****************************************

Na Woinde shizza , ARUSHA

Wanafunzi wanaomaliza  elimu ya kidato Cha sita wametakiwa kuchagua taaluma ambazo wakitokea wamekosa ajira ,waweze kujiajiri wenyewe.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari  Edmond rice,ambaye pia ni mkufunzi wa chuo kikuu Cha SAUT wakili Emanuel Sood wakati akiongea katika mahafali ya 14 ya kidato Cha sita yaliyofanyika shuleni hapo juzi.
Alisema kuwa kutokana na tatizo la ajira hapa nchini ni vyema wanafunzi wakasoma fani ambazo iwapo hawata ajiriwa na serikali au kampuni binafsi pindi wanapomaliza shule ,waweze kujiajiri wenyewe na kuajiri wenyewe.
“Nivyema kila mwanafunzi akasoma kitu ambacho kitamsaidia kujiajiri na nivizuri hapa shuleni mnapewa elimu ya nadharia pia vitendo ,hivyo elimu mnayoipata hapa mnaweza kwenda kujiajiri pindi mnapotoka hapa ,pia sio kujiajiri tu pia inasaidia kuwaajiri na wengine ,pia mkiwa uko majumbani msipende kukaa mtaani na kutembeza vyeti badala yake nitumie elimu mliopewa ,mliofundishwa mashuleni kujiajiri”alibainisha Sood
Kwa  upande wake mgeni rasmi wa mahafali hayo ambaye ni mkufunzi wa chuo kikuu Cha Nelson Mandela kilichopo mkoani hapa Prof. Verdiana Grace Masanja alisema kuwa  kutokana na swala la elimu bure wanafunzi wengi wamekuwa wakisoma na kufaulu ,hali iliopelekea ajira kuwa chache haswa serikalini hivyo ni vyema mwanafunzi akisoma ajuwe kabisa anasoma ili akajiajiri mwnyewe na sio kutegemea kuajiriwa pindi anapomaliza.
Aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa namna wanavyowafundisha wanafunzi elimu ya natharia na vitendo na kubainisha kuwa elimu hiyo itawasaidia Sana wanafunzi wanapomaliza shule pindi wanapoenda mitano kwani watakiwa wamepata elimu na ujuzi wa aina mbalimbali utakao wawezesha kuendesha maisha yao .
Aliwasisitiza wanafunzi hao kusoma zaidi masomo ya hisabati kwani katika  dunia tunayoelekea hamna kazi yoyote ambayo itafanyika bila kutumia hesabu ,ukiendana na sera yetu ya Tanzania ya viwanda .
“Serikali yetu imewekeza Katika mambo mengi na mambo yote yanategemea hesabu ,kila kazi utakayo fanya itategemea hesabu ,na huku tunapoenda ajira zitakuwepo lakini pia zitaitaji hesabu ukiangalia tu kwa mfano reli yetu itakapo kamilika itaitaji wafanyakazi lakini Ili uajiriwe lazima ujue hesabu,tukija kwenye mabomba ya mafuta ,msenge na mengineyo”alisema Masanja 
Nae mkuu wa shule ya sekondari Edmond rice Simon Kaswahili alisema kuwa jumla ya wanafunzi 165 wamehitimu kidato Cha sita na Kati yao wanafunzi 63 ni wasichana na wanafunzi 102 ni wavulana .
Alisema shule yao inafaulisha kutokana na uongozi wao kusimamia sera za ulinzi wa mtoto ,ambayo inasaidia kuwafundisha watoto nithamu na pindi wanapotoka shule hapo wanakuwa na heshima ,wanajieshimu ,ambapo pia aliwataka wanafunzi waendeleze  mazuri yote ambayo wameyapata shuleni hapo.