Home Siasa YOHANI LEONCE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA UVCCM HANANG’

YOHANI LEONCE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA UVCCM HANANG’

0
*****************************************
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Hanang’ Mkoani Manyara, wametimiza kiu yao kubwa ya kumpata mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo baada ya kusubiri kwa miaka kadhaa sasa.
Akizungumza wakati wa kufunguo mkutano huo mkuu wa Uvccm Hanang, Mgeni rasmi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang Ndugu Samwel Hhayuma Xaday ameendelea kuwambusha vijana wote juu ya Umuhimu wa kumchagua kiongozi wa Vijana anayetokana na Vijana wenyewe atakaebeba maono na matamanio ya vijana wote bila kuyumbishwa kwani kwa kufanya hivo mtakua mmepata sauti yenu katika vikao mbalimbali vya maamuzi na kuwainua vijana wengi zaidi kufikia ndoto zao.
“Ninaomba baada ya kukamilika kwa uchaguzi huu mwenyekiti atakayepatikana anipe mpango kazi wenu ili nijue namimi nashiriki vipi kukamilisha ndoto na matarajio yenu mliojiwekea. Hamasa ya vijana, michezo na ajira kwa vijana wetu bado sio ya kuridhisha sana” aliongeza Mh Hhayuma.
Wagombea katika uchaguzi kwa nafasi mwenyekiti na kura walizopata ni kama Ifuatavyo.
1.Angel Nicolaus 19
2.Desderi Dismas 32
3.Elifido Daffi 10
4.Eng Timoth Caroly 4
5.Joseph Ginawe 61
6.Masweti Africanus 5
7.Yohani Leonce 262
Baada ya msimamizi wa uchaguzi kumtangaza mshindi ndugu Yohani Leonce amewashukuru wajumbe wote na kuwaahidi kuendelea pale tulipoishia ikiwa ni pamoja na Kuhakikisha upatikanaji wa Jengo la Katibu na Kufufua ari na hamasa kwa vijana wote kwa kuanza na ziara maalum ya kuwafikia mahali walipo.
“Niwaombe wagombea wenzangu tushikamane kwa pamoja na yale mawazo yote mliokuwa mnatamani kila mmoja wetu nitayatekeleza kwa nguvu zangu zote,” amesema Leonce.
Tunawashukuru sana wasimamizi wa Uchaguzi huu katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa Mwl Jacob Siay kwa usimamizi wa uchaguzi uliotuka.