Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ( wanne kutoka kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali za maziwa zinazozalishwa na Kampuni ya Tanga Fresh alipotembelea kukagua shughuli za Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Tanga mapema leo Februari 27, 2021
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) akiangalia Ng’ombe waliopelekwa katika Mnada wa Nderema kwa ajili ya kuuzwa. Naibu Waziri alitembelea mnada huo uliopo Katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo Februari 27, 2021 kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika Mnadani hapo.
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wapili kulia) walipokutana katika kikao cha Wavuvi na Naibu Waziri huyo kilichofanyika Mkoani Tanga mapema leo Februari 27, 2021. Lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero za Wavuvi wa Mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara aliyenunua Ng’ombe katika Mnada wa Nderema uliopo katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo Februari 27, 2021. Naibu Waziri alitembelea mnada huo kukagua shughuli zinazoendelea katika mnada huo.