Home Michezo FISTON AIPELEKA YANGA 16 BORA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

FISTON AIPELEKA YANGA 16 BORA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

0

…………………………………………………………………………….

Timu ya anga  imetinga Hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ken Gold kutoka Chunya Mkoani Mbeya  Mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Yanga ni mshambuliaji kutoka Burundi Fiston Abdul kwa Mkwaju wa Penalti dakika ya 40 baada ya beki wa Ken Gold Boniface Mwanjonde kuunawa mpira ndani ya 18 na Mwamuzi Hamed Arajiga kutoka Manyara kuamua ipigwe Penalti.

Akitoa benchi Carlos Carlinhos alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 81 kwa kumpiga mchezaji wa Ken Gold kadi ambayo haikuwa na na madhara.