Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akipata maelezo kutoka kwa Injini Amos Kaihula Meneja Mwandamizi Usafirishaji Umeme Shirika la Umeme Tanzania Tanesco wakati alipokuwa akimpa maelezo alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho.
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akipata maelezo kutoka kwa Injini Amos Kaihula Meneja Mwandamizi Usafirishaji Umeme Shirika la Umeme Tanzania Tanesco wakati alipokuwa akimpa maelezo alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho eneo la kuendesha mitambo.
Baadhi ya mitambo iliyokwisha simikwa kwa ajili ya kupoza umeme kwenye kituo cha Dege Kigamboni.
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akipata maelezo kutoka kwa Injini Amos Kaihula Meneja Mwandamizi Usafirishaji Umeme Shirika la Umeme Tanzania Tanesco kulia wakati alipokuwa akimpa maelezo alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Waziri wa Sayansi na Tekinolojia Dk. Faustine Ndugulile
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akipata maelezo kutoka kwa Injini Amos Kaihula Meneja Mwandamizi Usafirishaji Umeme Shirika la Umeme Tanzania Tanesco wakati alipokuwa akimpa maelezo alipotembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Waziri wa Sayansi na Tekinolojia Dk. Faustine Ndugulile na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la a Umeme Tanzania Tanesco Dkt.Tito Mwinuka.
Picha ya Pamoja.
………………………………………
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),kuhakikisha linajenga lenyewe vituo vya kupoza umeme wa gridi ya Taifa kwa kutumia wahandisi wake ili kuleta tija na kujenga uwezo wa shirika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini.
Dk Kalemani ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Dege cha kupoza na kusambaza umeme wa gridi ya taifa wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao uko mbioni kukamilika na umepangwa kuzinduliwa rasmi Februari 28, mwaka huu .
Amesema mradi huo ni mkubwa ambao unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 28.2 utaondoa kabisa tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika wilaya nzima ya Kigamoni utawapa fursa wateja wote wapya ili kuwaunganishia hasa wale ambao tayari walishalipia gharama za kuvuta umeme lakini bado hawajafungiwa na wateja wapya.
Kalemani amesema “Nilitoa agizo ifikapo Februari 28 mwaka huu muwe mmemaliza ujenzi wa kituo hiki na nashukuru naona mmeenda vizuri katika siku hizi chache zilizobaki ni wazi mtamaliza jambo kubwa hapa ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi nakuongeza nguvu kazi.
Katika hatua nyingine alilitaka shitika hilo kuanzia sasa wajipange na miradi yote ya ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme wa gridi ambavyo wataalam wa shirika hilo wana uwezo wa kuvijenga na kufunga vifaa, wafanye kazi hizo peke yao badala ya kuwapa kazi hiyo wataalamu wan je.
“Wito wangu kuanza sasa sitaruhusu tena kmandarasi kutoka nje aje kujenga vituo vya kupoza na kusambaza umeme ambavyo nyie wataalam wa Tanesco mna uwezo wa kuvijenga, watumieni wataalam wenu kazi ya vifaa vinavyonunuliwa nje ibaki kwa vile ambavyo havipatikani hapa ndani’’,alisema Dk Kalemani.
Akizungumzia bei na jinsi serikali ilivyojipanga kuwasambazia wananchi umeme hususan maeneo ya pembezoni, Dk Kalemani alisema maeneo yote yaliyopitiwa na mradi wa umeme wa Rea , wananchi wanapaswa kulipia gharama ya Sh 27,000 kwa ajili ya kuunganishiwa umeme na sio zaidi ya hapo.
Dk. Kalemani Amesema hayo yametokana na mapitio mapya yaliyofanywa mwaka 2017 na 2019 ambapo serikali ilianisha maeneeo yanayopaswa kutozwa bei hizo hata yale yaliyopo sehemu ya mjini, miji na majiji lakini yako pembezoni na miradi ya REA imepita.
Ameongeza kuwa hata kama umeme unaosambaza sio wa REA, lakini eneo hilo kuna mradi wa REA umepita wananchi wote wenye uhitaji wa nishati hiyo wanapaswa kutozwa Sh 27,000 tu gharama za maombi ya kuunganishiwa umeme.
Ameitaka Tanesco kuanza kutumia nguzo za zege ili kuondokana na matatizo ya kukatika umeme mara kwa mara kwenye maeneo korofi.