Home Michezo YANGA YAINYUKA MTIBWA SUGAR BAO 1-0, CARLINHOS AWA SHUJAA

YANGA YAINYUKA MTIBWA SUGAR BAO 1-0, CARLINHOS AWA SHUJAA

0

**********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Yanga leo imepata ushindi baada ya mechi kadhaa za nyuma kuambulia sare ambapo leo ameichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Yanga ilionesha kuutawala mchezo licha ya kutofika kwenye lango la upinzani katika kipindi cha kwanza.

Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa na kuwaingiza wachezaji ambao walionesha hali ya kuutaka ushindi ndipo dakika ya 73 kiungo mshambuliaji Carlos Carlinhos aliiwezesha klabu yake kupata bao.