Baadhi ya wateja wa kinywaji cha Smirnoff Ice wakifurahia kinywaji hicho baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kukirudisha tena sokoni baaya ya kuwa hakipatikni kwa muda. Hafla ya kutangaza kukirudisha sokoni kinywaji hicho ilifanyika jijini Dar jana
Msaani wa kikazai kipya Jux, akitoa buriudani safi kwa watumiaji wa kinywaji cha Smirnoff Ice waliojitokeza.
……………………………………
Na Mwandishi Wetu Watumiaji wa kinywaji cha Smirnoff Ice Black wana kila sababu ya kufurahi baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kukirudisha sokoni kinywaji hicho kilichokose ambacho hakikuwepo sokoni kwa kipindi Kikiwa ni kinywaji kilichopo tayari kutumika klichochanganywa na Vodka na ambacho ni sehemu ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni mama ya SBL,
Diageo, Smirnoff Ice Black ilizinduliwa kwa mara nyingine kwa kishindo ambapo wateja walipata fursa ya kukionja na kukifurahia.Akiongea wakati wa uzinduzi huo, meneja uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus alisema kinywaji hicho sasa kitakuwa kinapatikana kila sememu na kuwataka watumiaji wake kuendelea kukifurahia.
“Baada ya kusubiri kwa muda, sasa tumewaletea tena kinywaji hiki cha kimataifa ili muweze kuendelea kukifurahia. Ni kinywaji chenye ladha nzuri nay a kipekee ambayo unaweza kuifurahia na marafiki,” alisema.
Bertha alisema pamoja na kuwaburudisha watumiaji wake, Smirnoff Ice Black imekuwa ikiunga mkono jitihada za kuendeleza vipaji mbali mbali vya vijana ikiwa ni pamoja na shindano la kusaka vipaji vya Ma-DJ wachanga ambapo tayari limeshafanyika mara tatu kipindi cha Nyuma.
“Kikiwa pia ni kinywaji kinachounga mkono ukuzaji wa vipaji, baada ya kurudi sokoni tutakwenda mbali zaidi kwa kuunga mkono siyo tu kutafuta Ma-DJ bali hata vipaji vingine na kwa hiyo vijana wa Kitanzania waendelea kufuatilia kwa ukaribu ili waweze kusikia na kupata fursa kutoka Smirnoff Ice Black,” alisema