********************************************
Lori la mafuta lililokuwa limebeba petrol na Dizel Lita elfu ishirini (20) lenye namba za usajiri T439 BNS Mali ya kampuni ya Petrol Africa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Wilayani Sumbawanga limedondoka eneo la Mangae Wilayani Mvomero Kilometa 50 kutoka Mjini Morogoro na kusababisha mtu moja kujeruhiwa pamoja na mafuta kumwagika huku Jeshi la Zima Moto likifanikiwa kuzuia madhara mengine yasitokee katika eneo la ajari hiyo.