Home Michezo TAIFA STARS YATOKA SARE 1-1 KWENYE MECHI YA KIRAFIKI

TAIFA STARS YATOKA SARE 1-1 KWENYE MECHI YA KIRAFIKI

0

********************************************

AYOUB Lyanga nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amefunga bao liliweka usawa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo, uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Lyanga alifunga bao hilo dakika ya 57 kipindi cha pili baada ya DR Congo kutangulia kufunga bao la kwanza kipindi cha kwanza.

Congo ilipachika bao dakika ya 19 kupitia kwa Fiston Mayela ambaye alipiga shuti kali akiwa nje ya 18 na mlinda mlango Juma Kaseja alikwama kuokoa baada ya kuteleza kabla ya kuokoa mpira uliozama wavuni.

Pongezi kwa Ditram Nchimbi aliyetoa pasi ya bao iliykutana na Lyanga ambaye aliwanyanyua mashaki dakika ya 57 Uwanja wa Mkapa.

Pia mkongwe Agrey Morris aliweza kutumia dakika 2 kwenye mchezo wa leo ikiwa ni mara yake ya mwisho kutumika ndani ya Stars baada ya kuomba kustaafu.

Kocha Mkuu wa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa wachezaji wake wengi ni wapya jambo linalomfanya ajenge muunganiko mzuri wakati ujao.