Home Makala SIMBA WALIFANIKIWA WAPI?

SIMBA WALIFANIKIWA WAPI?

0

************************************************

Na:Fadhila Kizigo

Kukubali kosa sio ujinga ila ni kujitambua nakujua kuwa wewe sio malaika ambaye ujawahi kumkosea mtu hata katika vitabu vyetu vya dini tunashauriwa kukubali kosa na kutubia toba ya kweli kweli ili Mungu akusamehe jumla jumla wewe ni nani usikubali kosa na kujua wapi ulikosea ili uanze upya.

Improvissation, Kuwatumia full back Shomari Kapombe na Mohamed Hussein kwenye kufanya mashambulizi kwenye hili wamefanikiwa mara zote mipira mingi ilipitia kwao na kuwalazimisha Fc Platnum kufanya makosa yaliowagharimu kwenye hili nilizungumza kabla ya mechi kuanza kuwa Kapombe na Mohamed Hussein ni sehemu ya ushindi wa Simba kwani walishambulia kitimu kwa kuumiliki mpira wakati wote na kuwafanya Fc Platnum kulazimika kufanya makosa mengi kupelekea penant mbili zilizopatikana lakini pia walifanikiwa kuhakikisha wanatoa pass ya kusurprise kwa wakati sahihi na kulekea ushindi kwenye hili kocha Sven amefanikiwa.

Mobiliy pass mara zote Simba walishambulia kwa kutumia pass za kuama kutoka kwa Mickson kwani ana speed akiwa na mpira na anauwezo wa kudribbling akienda kushambulia kwenye hili wamefanikiwa kwani muda wote Mickson alikuwa na speed iliyohusishwa na move ya mpira.

Penetration pass imezoeleka hii kwa Simba mara zote hushambulia kwa kutumia pasi mpenyezo Cloutus Chama amekuwa bora sana kwenye mashambulizi ya aina hii lakini pia Bwalya alikuwa bora sana kwenye shambulizi la aina hii hata magoli yaliyopatikana wamehusika kwa maana ya deep pass zimehusishwa na Bwalya na Chama kwenye hili wamefanikiwa.

Concetration kwenye back line ya Simba licha ya kuwa mechi ya kwanza walifanya makosa kwenye eneo la ulinzi lakini hawakurudia makosa yale ya Zimbabwe mara zote walikuwa bora walinzi wa Simba licha ya kushambuliwa lakinu walizingatia man marking defence on the formation ,covering goal na man
to man marking .

Sven ameamua mchezo na kuwavusha Simba kwenye hatua ya makundi kwa kubadilika kutokana na mchezo unavyohitaji kuna wakati Simba wakiongoza mbili Fc Platinum waliamka na pressure ilikuwa kwa Simba ubora wa kocha ni sehemu ya ushindi wa Simba kwa kutumia mbinu zake Simba wamefika hatua ya makundi kongole kwa Sven.

Imeandaliwa Na:Fadhila Kizigo Kocha Mwandishi 0673854979 Instragram fadhilakizigo19