*****************************
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene amewataka watumishi nchini kuendelea kutumia Mabaraza ya wafanyakazi kama chombo cha kupanga mipango ya kazi kwa taasisis husika na kutatua changamoto za kiutendaji badala ya kubeza mabaraza hayo.
Waziri Simbachawene aamesema hayo leo wakati akifungua kikao cha kumi na tatu cha baraza la wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kinachofanyika jijini Dododma ambapo alisemna kuwa, watumishi na watendaji wengine waliopo ndani ya Jeshi hilo wameendelea kufanyakazi nzuri hasa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, baraza limedhamilia kujadili kwa kina utekelezaji uliofanyika kwa manufaa ya jeshi hilo katika kuhakikisha usalama wa raiamali zao.