Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ( kushoto) akisaini kitabu cha wageni leo alipoanza ziara ya kikazi Iringa. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda ofisini kwake.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akikagua skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi wilaya ya Iringa ilinayokarabatiwa na Jeshi la Magereza chini ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufuatia kubomolewa na mvua hali iliyosababisha mto kuacha njia yake ya asili.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akikagua skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi wilaya ya Iringa ilinayokarabatiwa na Jeshi la Magereza chini ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufuatia kubomolewa na mvua hali iliyosababisha mto kuacha njia yake ya asili.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ( kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesera ( kushoto ) wakati alipowasili Pawaga kukagua skimu za umwagiliaji leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiongea na wakulima wa kijiji cha Isele kata ya Mlenge tarafa ya Pawaga leo alipotembelea kukagua skimu za umwagiliaji zilizoharibiwa na mvua ambapo ameahidi kuwa Tume ya Umwagiliaji itazikarabati zote ili wakulima waendelee kuzalisha mazao kwa wingi na ubora.
( Habari na Picha na Wizara ya Kilimo)
……………………………………..
Serikali imewatoa hofu wakulima wa mpunga wa mkoa wa Iringa kuwa wataendelea kuzalisha mazao kwa kutumia skimu za umwagiliaji baada ya ukarabati unaoendelea.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa leo (10.12.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alipokagua skimu iliyoharibiwa na mvua ya Mkombozi kijiji cha Itunundu wilaya ya Iringa alipofanya ziara ya kikazi.
Kusaya amekagua mfereji unaokarabatiwa na Jeshi la Magereza kwa kuweka mawe na mchanga ili kurudisha njia ya mto mahala pake kufuatia mvua nyingi zilzoharibu mwaka jana.
” Skimu hii ya Mkombozi yenye ukubwa wa hekta 12,000 ambayo mfereji wake ulibomolewa na mvua tutaikarabati mapema kwa kutumia fedha za serikali ,hivyo wakulima jipangeni kuendelea kulima” Kusaya alisema
Katibu Mkuu Kusaya aliongeza kusema wizara ya kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itaendelea kukarabati skimu zote nchini ikiwemo za kijiji cha Mlenge,Pawaga na zile za Ruaha Mbuyuni ili wakulima wazalishe zaidi.
” Lengo la Wizara ya Kilimo ni kuweka mindombinu ya kisasa kwenye skimu za umwagiliaji tukiamini ndio njia ya kkumkomboa mkulima kwa uhakika badala ya kutegemea mvua ,tutumie mito na mabonde kumwagilia ” alisisitiza Kusaya.
Kwa sasa Kusaya alisema mashine na mitambo ya kukarabati miundombinu ya umwagiliaji iliyoharibika ipo Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo ikimaliza kazi ya kurejesha mto kwenye eneo lake ili maji yaendelee kusambaa kwenye mashamba na ikimalizika mitambo hiyo itapelekwa Pawaga .
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Happiness Seneda aliishukuru Wizara ya Kilimo kwa hatua zake za kutoa shilingi Milioni 300 zinazotumika kukarabati miundombinu iliyoharibika .
” Kwenye sekta ya kilimo mkoa wa Iringa tumejipanga vema na kuwa tuanomba wizara iendelee kutusaidia kukamilisha ukarabati wa skimu zilizoharibika na mvua ” alisema Seneda.
Katibu Mkuu Kusaya anaendelea na ziara ya kikazi kwa kutembelea skimu za Ruaha Mbuyuni na kukabidhi ghala lililojengwa kwa ajili ya wakulima wa kijiji cha Isele wilaya ya Iringa kusaidia kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya .