Home Uncategorized KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA MRADI WA SGR AKIONGOZANA NA WAANDISHI...

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA MRADI WA SGR AKIONGOZANA NA WAANDISHI NA WASANII

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli TRC Bw. Masanja Kadogosa wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa treni ya Umeme SGR kipande cha Dar- Moro akiongozana na waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali leo Ijumaa Oktoba 16,2020.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-MRADI WA SGR)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akiongozana na baadhi ya waandishi wa habari na wasanii akikagua ujenzi wa kituo kikuu cha treni ya Umeme SGR eneo la Stesheni jijini Dar es salaam leo.

Masanja Machibya Meneja Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Umeme SGR kipande cha Dar- Moro akitoa maelezo ya namna utekelezaji wa mradi huo unavyoenda kwa waandishi wa habari na wasanii waliotembelea mradi huo leo.

Muonekani wa jengo la Stesheni kuu ya Reli ya Umeme SGR aneo la Posta jijini Dar es salaam.

Njia ya Reli hiyo inavyoonekana kwa juu katika eneo la kituo kikuu Stesheni jijini Dar es salaam.

  Baadhi ya wataalamu kutoka kampuni ya ujenzi ya Yapi Merkezi wakiwa kazini katika kituo hicho eneo la Stesheni jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wasanii na waandishi wa habari wakitembelea mradi huo katika eneo la stesheni jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli TRC  wakati alipotembelea mradi huo leo akiongozana na waandishi wa habari na wasanii mbalimbali alipotembelea mradi huo leo katika eneo la kituo0 kikuu cha stesheni jijini Dar es salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari na wasanii mbalimbali wakitembelea mradi huo eneo la kituo kikuu cha treni ya Umeme SGR Stesheni jijini Dar es salaam.