Washiriki zaidi ya 300 wameshiriki mbio fupi za kilomita 5 katika bonde la Olduvai Ngorongoro kwa lengo la kutangaza vivutio vya asili vya Olduvai na Laetoli ambapo historia ya Binadamu wa Kale ilianzia.

Akizungumza kwa Niaba ya Kamishna wa Uhifadhi kwenye tukio hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa

Ngorongoro kwa kushirikiana na Cape to Cairo Marathon imefanya mbio hizo ili kuonesha utajiri wa utalii wa asili, historia, urithi wa utamaduni na mambo kale uliopo Olduvai na Laetoli kama Nyumbani kwa asili ya Binadamu. Ameongeza kuwa Ngorongoro ni Nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kwa kuwa pumzi ya kwanza ya ndama kupigwa mhuri kabla ya kuhamia maeneo mengine safari yao huanzia Ndutu Ngorongoro.

“Ngorongoro ni Nyumbani kwa asili ya binadamu kisayansi, Ni nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kila mwaka, ni nyumbani kwa Spinshi ya Ndege zaidi ya 500, ni nyumbani kwa Wanyama wakubwa watano, kiufupi eneo la Ngorongoro ni Nyumbani kwa mkusanyiko wa Vitu vingi ndio maana tunawaambia wadau wote ndani na nje ya Nchi kuwa Wonders Are Calling” ameongeza Kamishna Kobelo.

 Mkurugenzi wa Cape to Cairo Arusha International Marathon, Timothy Mdinka ameeleza kuwa lengo la mbio hizo ni kutangaza mazao mapya ya Utalii yaliyopo Tanzania na Bara la Africa kwa Ujumla kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo Michezo kama mbio ambayo imefanyika leo Olduvai pamoja na marathon ya Cape to Cairo itakayofanyika tarehe 31 Mei, 2026.

Mbio hizo zimejumuisha wadau mbalimbali wakiwepo Ngorongoro, Cape to Cairo international Marathon, Karatu Runners, Amani Collection, CRDB, UNDP, NHIF, Diplomatic and Tourism Police Arusha