Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi Kigwa Igalula nkoani Tabora akiwa njiani kuelekea Dodoma leo Jumanne Septemba 22, 2020.
Rais Dk John Pombe Magufuli amewasisitizia wananchi kuachana na vyama vinavyopanga kuigawa nchi katika majimbo kwani vyama hivyo havina nia njema na Taifa vinataka kuleta mifarakano kwa watanzania kwa sababu utawala wa majimbo utawagawa wananchi na kuleta mgawanyiko mkubwa kwa taifa.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-IGALULA TABORA)
Mussa Ntimizi aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igalula akimuombea kura Rais Dlk. John Pombe Magufuli alipozungumza na wananchi wa Igalula Kigwa.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Igalula mkoani Tabora Bw. Venant Protas akimuombea kuraRais Dk. John Pombe Magufuli na yeye katika mji wa Igalula.
Picha mbalimbali zikionesha wananchi waliojitokeza kumlaki mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. JOhn Pombe Magufuli katika mji wa Igalula mkoani Tabora.