……………………………………………………….
Na Masanja Mabula ,Pemba.
MAHAKAMA ya mkoa wa kaskazini pemba imempeleka rumande mzee Nassor Ali Hamad mwenye umri wa miaka 65 kwa tuhuma za kutorosha na kulawiti.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo , mwendesha mashtaka wa serikali Seif Mohamed Khamis aliiambia mahakama kwamba tarehe 28 julai mwaka huu 2020 mtuhumiwa huyo inadaiwa alimtorosha na kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 14 jina linahifadhiwa.
Amesema kwamba kosa la kwanza la kutorosha ni kinyume na kifungu cha 113 (i)(b) cha sheria namba 6/2018 sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“ Kosa la kwanza la kutorosha ni kinyume na kifungu cha 113 (i),(b) cha sharia namba 6 /2018 sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar’’amesema.
Seif amefahamisha kwamba kosa la pili la kulawiti ni kinyume na kifungu cha 115 cha sheria namba 6/2018 sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baada ya kusomewa makosa hayo , mtuhumiwa amekana kufanya makosa hayo na kuiomba mahakama impe dhamana jambo ambalo limekataliwa kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana kisheria.
Kwa hiyo mtuhumiwa huyo amepelekwa rumande hadi tarehe 8 mwezi ujao kesi hiyo itakapokuja kuanza kusikilizwa upande wa mashahidi.
Hivyo hakimu wa mahakama hiyo aliamua kuipangia tarehe na kuagiza mashahidi wote waitwe kwa ajili ya kutoa ushahidi.