Home Siasa DKT. SHEINI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU ...

DKT. SHEINI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA ZANZIBAR

0
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
……………………………………………………………….
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo Augost 27 mwaka 2020, ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. 
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 9:00 Asubuhi. 
Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa ya mapendekezo ya Wana CCM walioomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, kutoka katika Majimbo na nafasi ya Uwakilishi Viti Maalum vya Wanawake katika Mikoa ya Zanzibar.
Kikao hicho ni maalum kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 na 109  (1), (7). 
Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM.