********************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
Katibu wa UVCCM Mkoani Pwani, Christina James ,amesema wakati chaguzi za ndani ya Chama Cha Mapinduzi zikimalizika ni vyema wanachama wakaondokana na makundi na kuachana na visasi.
Akisimamia zoezi la kura za maoni ,kata ya Mailmoja ameeleza, makundi yanaweza kuzalishwa wakati wa uchaguzi lakini kipindi hicho kikiisha wanapaswa kuwa na umoja ili kusaka ushindi wa chama katika uchaguzi mkuu.
Christina amewaasa wanaCCM kuwa kujenga fito moja na kuwa na upendo na mshikamano kukiimarisha chama.
Ametangaza kuwa kura za maoni kata ya Mailmoja ametamba Ramadhan Lutambi kwa kupata kura 75 ambapo ametetea nafasi hiyo ambayo ameishika kwa miaka mitano iliyopita,akifuatiwa na Christopher Mjema aliyepata kura 47.
Matokeo kata ya Pangani ameshinda Augustino Mdachi aliyeongoza kwa kura 59 akifuatiwa na
Amir Msangi kura 27.
Matokeo kata ya Sofu ,ameongoza Mussa Ndomba 33 akifuatiwa na Yusuph Mbonde kura 15, kata ya Misugusugu ameongoza John Mwinami-42, Kata Ya kibaha Manyama kura 44 ambapo kata ya Visiga ameshinda Kambi Legeza aliyejinyakulia kura 79 .
Kata ya Mbwawa Matokeo Junneth Mruge ameshinda kwa kura 33, na kata ya Kongowe ameibuka mshindi Hamis Shomari ambae kapata kura 84 akifuatiwa na Iddi Kanyalu aliyejiokotea kura 43.