“Tunajivunia sana kuwa sehemu ya ligi kuu ya Tanzania bara kwani inaendelea kukua na kuboreshwa mwaka hadi mwaka. Pongezi zetu pia ziwaendee viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , bodi ya ligi , vilabu vyote shiriki, waandishi wa habari, wadhamini wenza pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika ligi kuu mwaka huu,” Linda Riwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom alisema.
Mpira wa miguu ni mchezo pendwa na muhimu sana hapa nchini na duniani kote.
Hii ni katika kuwapa burudani wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla, kutoa nafasi za ajira kwa wachezaji na watendaji pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa jamii na nchi tofauti. Mtandao wa Vodacom umekuwa mstari wa mbele katika kuwaunganisha na kuwaleta pamoja Watanzania kupitia mtandao namba moja na wenye kasi zaidi hapa nchini. Vodacom inasifika kwa kutoa huduma bora zaidi za data , kupiga simu, sms na mpesa.
“Kama mnavyojua mpira wa miguu ni fursa kubwa ya ajira kwa vijana na tunafurahi na kujivunia kuwa sehemu ya mafanikio tunayoyaona kutokana na udhamini wetu ambao umewezesha baadhi ya wachezaji kama Mbwana Samatta na Simon Msuva kupata fursa za kucheza nchi za nje na kufika ulaya,” aliongeza Linda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Vodacom kama wadhamini wakuu wa ligi kuu wametoa hamasa kwa klabu zote kuendelea kuwa mabalozi wazuri na kuwlezea nia ya kuendelea kutoa hamasa na ushirikiano kwetu kuendeleza michezo na hasa mpira wa miguu nchini.
Vodacom pia inatoa shukrani za dhati kwa Watanzania kwa kuendelea kujitokeza kushabikia timu zao maana mchezaji wa kumi na mbili katika timu yoyote ya mpira ni mashabiki. “Shukrani zetu kwa waandishi wa habari kwa mchango mkubwa wa kuwahabarisha wapenzi wa mpira wa miguu walio ndani na nje ya nchi na kutangaza ligi yetu ya Vodacom Premier League,” aliongeza Riwa