Naibu waziri wa Tamisemi Mhe. Josephat Kandege akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, Katibu Tawala Bi Stella Msofe pamoja na Mganga Mkuu Dokta Samweli Laizer wakati akikagua upanuzi wa Zahanati ya Bunju iliyopo katika Halmashauri hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akimuonesha Naibu Waziri wa Tamiseni Mhe. Josephat Kandege ujenzi wa mfereji wa kupitisha maji, mwenyeshati jeupe ni Meneja wa TATURA Leopord Runji.
Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Josephat Kandege akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pamoja na wakandarasi wanaojenga barabara ya Shekilango Bamaga wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo.
Muonekano wa ujenzi wa mfereji wa kupitisha maji.
Meneja wa TATURA Leopord Runji akimuonesha Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Josephat Kandege hatua inayoendelea katika ujenzi wa mfereji wa kupitisha maji.
Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Josephat Kandege pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe.Daniel Chongolo wakiangalia karavati za kuweka kwenye mifereji ya kupitisha maji.
…………………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege ameridhishwa na matumizi ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zilizotumika katika utekelezaji wa miradi ya maedeleo iliyokamilika kwa wakati na viwango.
Amesema kuwa Manispaa hiyo ni mfano wakuigwa kwa kuwa imeonesha nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha zinazotokana na vyanzo vya mapato ya ndani na kwamba miradi ambayo imetekelezwa kupitia fedha hizo inaendana na thamani halisia.
“Kimsingi leo nimemaliza ziara yangu katika Halmashauri hii, na kikubwa nilikuwa nimelenga zaidi kuona fedha zinazokusanywa na Halmashauri na namna ambavyo zinatumika katika miradi ambayo inaonekana na kimsingi naomba niwapongeze sana Kinondoni, mnazitendea haki fedha zenu mnazokusanya” amesema Mhe. Kandege.
Kadhalika Mhe. Kandege ameridhishwa na kiwango cha barabara zinazojengwa katika Halmashauri hiyo kupitia mradi wa DMDP na kusema kuwa kukamilika kwake kutaleta mafanikio makubwa kwa wananchi hususani watumiaji wa barabara ya Shekilango na kwamba itaondoa msongamano wa daladala na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya foleni.
Amefafanua kuwa Mafanikio haya yanayoonekana leo Kinondoni ni kutokana na uongozi imara wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi ndg. Aron Kagurumjuli ulioleta tija kwa Wananchi.
Katika hatua nyingine Mhe.Kandege ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kujenga kituo cha Afya katika Kata ya Kigogo na kusema kuwa walifanya mamuzi ya busara na yakujali wananchi kwakuwa eneo hilo halikuwa na Hospitali na kwamba litawasaidia wakazi hao kupata huduma bora ya afya.
“Kinondoni mliona mbali kuweka kituo cha Afya pale Kigogo, mlitumia busara ya hali ya juu mkaona ni bora mnunue eneo kwa ajili ya kuwajengea wananchi kituo cha Afya, hivyo hata kwenye Kata ya Kawe kwa ujumla ukiondoa Kawe kama Kawe eneo lililobaki halikuwa na kituo cha Afya, pamoja na ujenzi wa Hopsitali ya Wilaya nilazima uwe navituo hivi ili hata mgonjwa wa eneo jirani apate huduma.
Katika ziara hiyo Mhe. Kandege ametembelea Barabara ya shekilango inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa shilingi Bilioni 14. 8, mfereji wa Kilongawima uliyopo Jimbo la Kawe kwa shilingi Bilioni 3.1 pamoja na upanuzi wa Zahanati ya Bunju mradi unajongekwa cha shilingi Milioni 600.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Mahusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.