Home Mchanganyiko JPM ATIMIZA NDOTO YA WAKAZI WA MICHENGA MKOANI MOROGORO KWA KUWAPATIA UMEME

JPM ATIMIZA NDOTO YA WAKAZI WA MICHENGA MKOANI MOROGORO KWA KUWAPATIA UMEME

0

Na.Farida Saidy,Morogoro
Wananchi wa kata ya Michenga wilayani Kilombero Mkoani Morogoro wameishukuri serikali na Jemedari wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupatiwa umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) awamu ya tatu mzunguko wa kwanza, huduma ambayo hawajawahi kuipata tangu Nchi ipate uhuru.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na wakazi hao katika ziara ya kikazi ya Kamishna Msaidizi wa umeme wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga wakati akikagua miradi yote ya umeme vijijini katika wilaya za mkoa wa Morogoro ikiwa ni katika kufanikisha azma ya serikali ya kufikisha umeme vijiji vyote hapa nchini kwa kupitia Wakala wa umeme vijijini(REA).
Wakizungumza na Fullshangwe Blog wananchi hao akiwemo Bw Chanjala Meja,Mzee Salum Kimbwembwe (30) na Bi Magreth Mlungukauya wamesema hatua hiyo ya Serikali kuwapatia umeme itawaletea mabadiliko ya makubwa ya maendeleo ya kiuchumi.
Aidha wameipongeza serikali kwa hatua hiyo huku wakiahidi kuendelea kuipa ushirikiano serikali katika miradi mingine ya maendeleo ili kufikia maendeleo yanayotakiwa katika nchi .
Kamishna Msaidizi umeme wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga amesema kulijitokeza changamoto kazaa katika utekelezaji miradi lakini kwa sasa zimeshatatuliwa na mpaka sasa mradi unatarajia kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huku
MhandisiLuoga akiwa ziarani kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini amewasisitizia wananchi kutumia fursa ya kupata nishati hiyo kujiletea maendeleo ya kiuchumi kwenye maeneo yao.
“Sasa umeme ndio huu mmeletewa fanyeni kazi kama anavyosema Rais wate Dkt. John Pombe Magufuli nimeona hapa kuna mafundi selemala, saluni na mashine za kukoboa mpunga, basi naomba baada ya umeme huu kuwaka kila mtu achape kazi ili kuleta maendeleo katika eneo hili”, ametoa wito Mhandisi Luoga
Katika ziara Mhandisi Luoga