******************************
TUKIO LA KWANZA.
TAREHE 20.06.2020 MAJIRA YA 19:20HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA BUKELEBE, KIJIJI CHA KANYAMA, KATA YA BUJORA, WILAYA YA MAGU,AMBAKO ALIKAMATWA TUBETI MATIKO, MIAKA 24, MKURYA, FUNDI UJENZI, MKAZI WA KIJIJI CHA KANYAMA, KWA TUHUMA ZA KUMUUA BAADA YA KUMCHOMA KISU KIFUANI NA KUMSABABISHIA KIFO MAHIGE CHACHA, MIAKA 24, MKURYA, FUNDI UJENZI, MKAZI WA KIJIJI CHA KANYAMA. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALITEKELEZA MAUAJI HAYO BAADA YA KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA ANAENDA MTONI KUOGA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA MAPENZI KWANI INADAIWA KUWA VIJANA HAO WALIKUWA WAKIMGOMBEA MSICHANA AMBAE JINA LIMEHIFADHIWA ILA NI MKAZI WA KITONGOJI CHA BUKELEBE. UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAKAMILISHWA NA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKANI HARAKA IWEZEKANAVYO , MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA SEKOU TOURE KWA UCHUNGUZI ZAIDI WA DAKTARI, NA UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
TUKIO LA PILI.
TAREHE 20.06.2020 MAJIRA YA 17:30HRS KATIKA BARABARA YA PAMBA YENYE MSONGAMANO WA WATU WENGI, GARI NAMBA T. 312 DFA AINA YA MITSUBISH FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAE LAMECK MMARI, MIAKA48, MCHAGA MKAZI WA BUHONGWA AKITOKEA ENEO LA SAHARA KUELEKEA PICHA YA MWALIMU KATIKATI YA MJI ALIWAGONGA WAFANYABIASHARA WALIOKUA WAMEPANGA BIASHARA ZAO KARIBU NA BARABARA PIA WATEMBEA KWA MIGUU NAKUSABABISHA VIFO KWA WATU WAWILI AMBAO NI:-
- MAYALA S/O, MIAKA 23, MSUKUMA, MFANYABIASHARA WA MANANASI, MKAZI WA MALIMBE.
- SOPHIA MASATU, MIAKA 38, MUHA, MKAZI WAMBUGANI, WOTE WAWILI WALIFARIKI DUNIA WAKATI WAKIENDELAEA KUAPTIWA MATIBABU.
MAJERUHI KATIKA AJALI HIYO NI SITA AMBAO NI ;-
- ROSEMARY WAMBURA, MIAKA 42, MNGULIMI, MKAZI WA MULEBA.
- TEDDY SAYI, MIAKA 28, MSUKUMA, MKAZI WA MJIMWEMA.
- CHRISTINA SYLIVESTA, MIAKA 16, MUIRAQ, MWANAFUNZI KIDATO CHA TATU KATIKA SEKONDARY YA IGOMA.
- FELISTER MABULA, MIAKA 16, MSUKUMA, MKAZI WA MJIMWEMA.
- JOSEPH DANIEL, MIAKA 29, MJITA, MKAZI WA BUSWELU NA
- ERIC RICHARD, MIAKA 24, MFANYABIASHARA WA VIATU, MKAZI WA MBUGANI.
AIDHA KATI YA MAJERUHI HAO WATATU WAMERUHUSIWA BAADA YA HALI ZAO KUENDELEA VIZURI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIA DEREVA WA GARI AITWAYE LAMECK MMARI KWA MAH JIANO NA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA KUWEPO KWA HITILAFU ZA BRAKE KATIKA GARI HILO NA UZEMBE ILA UCHUNGUZI WA KINA UNAENDELEA. MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALI YA BUGANDO KWA MATIBABU. HALI ZAO ZINAENDELEA KUIMARIKA, PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO KWA UCHUNGUZI WA DAKTARI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUWATAKA MADEREVA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI NA KUHESHIMU WATUMIAJI WANGINE WA BARABARA. PIA LINATOA RAI KWA JAMII HUSUSANI VIJANA KUTAFUTA NJIA SAHIHI YA KUTATUA MIGOGORO YAO HASA YA KIMAPENZI ILI KUJIEPUSHA NA MATUKIO YA KIJINAI YASIYO YA LAZIMA YANAYOPELEKEA KUJIKUTA WAKIWA MIKONONI MWA VYOMBO VYA DOLA.