Home Mchanganyiko WALIMU 40 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KUBORESHA UWEZO

WALIMU 40 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KUBORESHA UWEZO

0

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dk. Daniel Fussy akizungumza na vyombo vya habari.

 

Mkurugenzi wa HakiElimu nchini, Dk.John Kalage akizungumza wakati  wa kufunga mafunzo ya walimu 40 wa elimu ya awali yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Mkwawa Iringa.  

Baadhi ya walimu walioshirikia mafunzo ya kuwaongezea uwezo ikiwa ni Mradi huo uliopewa jina la Mwanzo Mzuri  wa miaka tatu na unafadhiliwa na UKAid kupitia Mfuko wa Ustadi wa Maendeleo ya Binadamu na huletwa kwa kushirikiana na HakiElimu, Chuo Kikuu cha VIA Chuo Kikuu cha Denmark na Chuo Kikuu cha Mafunzo cha Mkwawa.

*********************************

NA DENIS MLOWE,IRINGA

WALIMU 40 wa shule za awali wamenufaika na mafunzo yenye lengo la kuboresha uwezo na weledi wa walimu kitaaluma na kivitendo yenye nia ya kuchochea zaidi matokeo ya kujifunza kwa wanafunzi wa awali.

Mafunzo hayo ambayo ni Mwanzo Mzuri inatarajia kuhakikisha kuwa vijana wa Kitanzania wataandikishwa elimu ya hali ya juu na salama ya mapema, ambayo inaboresha utayari wa shule na kuwasaidia kufikia ufikiaji wao kamili katika kujifunza kwa wanafunzi wa awali.

Mradi huo uliopewa jina la Mwanzo Mzuri ni wa miaka tatu na unafadhiliwa na UKAid kupitia Mfuko wa Ustadi wa Maendeleo ya Binadamu na huletwa kwa kushirikiana na HakiElimu, Chuo Kikuu cha VIA Chuo Kikuu cha Denmark na Chuo Kikuu cha Mafunzo cha Mkwawa ikiwa na mlengo wa kujaribu mfumo mpya wa ubunifu unaozingatia watoto kwa elimu ya mapema ambayo itaboresha utayari wa shule na matokeo ya kujifunza kwa watoto wa miaka 0-6.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa walimu hao, Mkurugenzi wa HakiElimu nchini, Dk.John Kalage alisema kuwa mradi huo umeigemea katika uwekezaji katika miundombinu ya matokeo bora ya kujifunza, pamoja na vyoo, usambazaji wa maji, vyumba vya madarasa au bustani za jikoni na kuwezesha jamii na maarifa na muundo wa kushiriki, na kuendesha suluhisho kwa maswala ya ECD, pamoja na elimu, ukatili dhidi ya watoto (VAC), afya, na lishe;

 Aidha alisema kuwa mradi huo una lengo la kufuatilia utekelezaji wa sera na utetezi katika ngazi ya kitaifa na kitaifa kwa sera na miongozo itakayotoa elimu bora na ya awali ya msingi.

Dk. Kalage alisema kuwa mafunzo hayo  ya Kozi ya Nne ya Mradi wa Mwanzo Mzuri yana umuhimu mkubwa sana katika kuboresha uwezo wa walimu katika kuwawezesha wanafunzi kujifunza na kuwawezesha na kuongeza weledi wa walimu kitaaluma  na ki-vitendo,  na hivyo kuchochea zaidi uwezekano  wa  kuboresha matokeo ya kujifunza ya wanafunzi..

Alisema kuwa Mpango  huu    ulikuwa  ni  sehemu  utekelezaji  wa  Mpango  Mkakati  wa  Wizara  wa Kuendeleza na Kusimamia Walimu wa mwaka 2008  – 2013 (Teachers Development and Management Strategy (TDMS) ambapo mwaka 2017 Wizara ilitoa Mwongozo wa Mafunzo kazini kwa Walimu (National Framework For Continuous Professional Development Strategy  for  Practicing  Teacher).

 Alisema kuwa pamoja  na  jitihada  hizi  za  Serikali  sio walimu  wote  wamekuwa  wakipata  nafasi  ya  kujiendeleza  wakiwa  kazini  kutoka  na sababu  mbalimbali  ikiwemo  ufinyu  wa  bajeti  hivyo kama haki elimu kutokana na Utafiti    wa  “Mazingira  ya  Kujifunza  na  Kufundishia  ya Elimu  ya  Awali’    tuliouzindua  mwishoni  mwa  mwezi  May  2020  una  thibitisha haya.

Aliongeza kuwa kwa kutambua hilo HakiElimu kwa kushirikina na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa na Chuo Kikuu cha  VIA cha Denmark vilibuni mafunzo haya kwa walimu  wote  40  kupata mafunzo hayo ya awali kwa lengo la kuboresha elimu ya watoto wa awali.

“Tunatambua  kuwa,  serikali  na  wadau  wengine  pia  wamekuwa  katika  jitihada za kuwapatia walimu mbalimbali hapa nchini mafunzo kazini. Hata hivyo, sisi tunaamini mafunzo haya yana sifa ya ziada maana yanalenga kuwapatia mbinu za  kuwawezesha wanafunzi  kujifunza  kwa kuboresha  matendo  yenu  mnapokuwa  darasani.  Ni  wazi kwamba mwalimu anayejifunza nadharia kwa kuihusisha na vitendo halisi anakuwa na uwezo mkubwa zaidi katika ufundishaji na uambukizaji maarifa” alisema.
     
 Aliongeza kuwa Mafunzo hayo yenye kozi tano ambazo zimeandaliwa katika mtiririko maalumu unaotegemeana ikiwemo umuhimu  wa  kufanya uchunguzi  na  uandishi  wa  taarifa  ambazo  zitasaidia  katika  utendaji  wenu  wa  kila siku, michezo  na  Kujifunza ikiendana  na Mtaala  wa  Elimu  ya  awali  unaosisitiza  matumizi  ya  mbinu  ya michezo katika kufundisha na kujifunza.

Aidha mafunzo yaliyotolewa yalilenga kukuza  uwezo  wa wanafunzi  kujifunza kwa kushirikiana ili  kuwawezesha wanafunzi  kufikia  malengo  kwa  pamoja  na  kupunguza  mashindano  na  utengano na kozi nyingine kujenga uwezo wa kuwasaidia watoto kutumia  viungo vyao kutambua na kujifunza

Dk.Kalage alitoa wito kwa walimu hao kubuni  au kupendekeza  mbinu  muafaka  za    kukabiliana  na  changamoto ya  kufundisha madarasa makubwa na eneo la pili lenye changaamoto, ni utekelezaji wa elimu jumuishi ambapo serikali imeweka msisitizo mkubwa kupitia sera na mipango mbalimbali ya elimu.

Alisema kuwa kwa upande wao Ujumbe wa HakiEli elimu ya awali ina umuhimu mkubwa sana kwa kuwa ndiyo msingi wa wanafunzi  bora  vyuoni  na  viongozi  na  watendaji  mahiri  hapo  baadae hivyo tunapaswa kuipa umuhimu unaostahili na kila  mmoja  ni  muhimu  kuzingatia  nafasi  yake  katika  hili.

Aliongeza kuwa vyuo  ni  lazima  vijikite  na viazimie  kuzalisha  walimu  bora  na  watendaji  bora  watakaosimamia  elimu  ya  awali na Walimu  ni lazima wazingatie mafunzo  na wayatumie ipasavyo  kuwaandaa watoto na serikali ni lazima iweze kuwaunganisha na kuwatengenezea mazingira wezeshi wadau wote wa elimu ya awali zikiwemo shule   
 
Kwa upande wake, Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dk. Daniel Fussy kutoka chuo kikuu cha Mkwawa, alisema kuwa katika mafunzo ya awali waligundua kuwa kulikosekanika muungano kati ya walimu na wanafunzi hivyo mafunzo hayo yamewasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto hiyo.

Alisema kuwa  walimu wanatakiwa pindi wanafundisha muhimu sana kufanya uchunguzi kwa watoto na kubaini talanta walizonazo na kutowaacha peke yao pindi mafunzo yoyote yanapoendelea hivyo lazima kuandika taarifa kubaini mapungufu ya wanafunzi wa awali kwa lengo la kuwasaidia.