Uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza unawatangazia wananchi wote wenye sifa stahiki kutuma maombi ya Kujiunga na Chuo hicho kwa Ngazi ya Stashahada katika mwaka wa masomo 2018/2019. Chuo kimesajiliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa Usajili No.REG/PWF/019 na kina ithibati kamili (full accreditation). Chuo kinatoa Stashahada ya Michezo katika programu zifuatazo; Stashahada ya Elimu ya Uongozi na Utawala katika Michezo (Ordinary Diploma in Sports Management and Administration-ODSMA), Stashahada ya Ufundishaji Michezo (Ordinary Diploma in Sports Coaching Education- ODSCE) na Stashahada ya Elimu kwa Michezo (Ordinary Diploma in Physical Education and Sports – ODPES).
Sifa za kujiunga;
Muombaji anatakiwa awe na sifa zifuatazo;
1.1 Awe amehitimu kidato cha nne na kupata ufaulu usiopungua alama “D” nne (4) kati ya masomo aliyotahiniwa katika mtihani huo;
1.2 Awe amepata mafunzo ya cheti katika Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
1.3 Awe amepata mafunzo ya awali ya fani yoyote ya michezo au Elimu kwa Michezo au Sayansi ya Michezo kutoka mamlaka yoyote inayosimamia michezo na inayotambuliwa na serikali.
2.0 Kwa wahitimu wa kidato cha sita wawe na ufaulu usiopungua “Principal pass” moja na ”subsidiary” moja katika masomo aliyotahiniwa katika mtihani wa kumaliza kidato cha sita na uzoefu wa kushiriki katika michezo.
3.0 Wenye stashahada au shahada katika fani nyingine yoyote wawe na uzoefu wa kushiriki katika michezo.
1
Fomu za kujiunga zinapatikana Chuoni na kwa kupitia tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.habari.go.tz, na tovuti ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya
www.mcsd.ac.tz
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 6 Septemba 2018 saa tisa na nusu alasiri.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na ofisi ya Mkuu wa Chuo kwa anwani ifuatayo:-
Mkuu wa Chuo, Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, S. L. P 153, Ngudu, Kwimba – Mwanza. Simu Na. +255713403153, +255784403153, +255784389269 au +255767667828 Barua pepe: [email protected],[email protected]
IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA MICHEZO MALYA