Muonekano wa Ndani wa Masjd Abdulkarim Swabur uliojengwa Kitunda Machimbo Ukonga nyuma ya airport Dar es Salaam na Mtanzania anayeishi Canada Ukhuti Madina Abdulkarim baada ya kuzinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dar es Salaam
Mtanzania anayeishi Canada Ukhuti Madina Abdulkarim amemuenzi marehemu baba yake Alhaji Sheikh Abdukarim Swabury kwa kujenga Msikiti uitwao Masjid Abdulkarim Swabury ili kuhamasisha jamii kuzidisha ibada katika Maisha yao ya kila siku.
Ukhuti madina amebainisha hayo hivi karibuni katika uzinduzi wa msikiti huo uliyojengwa Kitunda Machimbo Ukonga nyuma ya airport Dar es Salaam wakati alipofanya mahojiano na mwandishi wetu wa kituo hiki kwa njia ya mtandao akiwa nchini Canada.
Aidha Ukhuti Madina amesema kuwa Masjid Abdulkarim Swabury ni sehemu ya kutambua mchango wa marehemu Alhaji Sheikh Abdulkarim katika kuhamasisha jamii kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kutanguliza ibada ili kuweza kufanyikisha shughuli zao ki halali.
“Natoa wito kwa jamii kufanya ibada kwa wingi ili kuliombea taifa na dunia kwa ujumla juu ya kupambana na janga la Corona “, ametoa wito Ukhut Madina.