Home Biashara Little inapanua Shughuli zake nchini Tanzania

Little inapanua Shughuli zake nchini Tanzania

0

LITTLE, Kampuni ya Taxi ya kimtandao inayotoa huduma za usafiri kwa wateja sasa imepanua wigo wake wa huduma rasmi- Dodoma,
Arusha na Mwanza ,hii ni kutokana na ongezeko kubwa la uhutaji , LITTLE ilianzisha huduma zake Dar es salaam, Tanzania 2019 , Ilikumuhakikisha urahisi, mteja atapaswa kulipia Shs 500/- kwa kilomita na Shs 80 kwa Dakika atakazotumia Akiongelea upanuzi huo ,Mkuu wa Operesheni Little Tanzania Eddsteve
Mwangalimi Alisema, “Maono ya LITTLE ni kuwa mtoa masuluhisho ya usafiri barani Afrika . Tumeshuhudia ongezeko kubwa la uhitaji wa huduma zetu katika nchi mbali mbali Tanzania ikiwemo , hii imepelekea kupanua wigo wa huendeshaji Dodoma , Arusha na Mwanza kutokata na uhitaji mkubwa wa huduma” LITTLE inatoa fursa kwa Madereva Taxi kujiongezea kipato zaidi ,tayari
tumeshasajiri Madereva Taxi zaidi ya 100 kila mkoa wakiwa tayari wamekwisha patiwa mafunzo katika viwango vyetu vyaki kampuni ili kuhakikisha ubora wa huduma unazingatiwa
Kampuni ya LITTLE ni ya Kiafrika iliyoanzia Kenya katika jiji la NairobiKenya, kampuni ipo katika nchi nne sasa ambazo ni Kenya,Tanzania, Uganda, na Zambia LITTLE inaendelea kutoa masuluhisho mbali mbali ya changamoto mbalimbali kwa aina ya kipekee na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma iliyo bora, rahisi na unafuu , Little App inapatikana Google play store na App Store.