…………………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Serikali imefanikiwa kujenga vituo vya afya 487, hospitali za wilaya 71, hospitali za Mikoa 10 na hospitali za Rufaa 3 ili kusogeza huduma za afya nchini kwa wanachi wake.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilihutubia bunge pamoja na kufunga shughuli za kibunge.
Rais Magufuli amesema kuwa watumishi wa afya zaidi ya elfu 14 wameajiliwa ili kwenda kuhudumu katika hospitali hizo na vituo vya afya ili watanzania kupata huduma bora.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa serikali imeboresha upatikanaji wa dwa baada ya kuongeza bajeti yake ili watanzania waweze pata dawa.
“Idadi ya wakinamama wa kujifungua imeongezeka katika vituo vyetu vya afya na kufikia asilimia 85 hiyo ikiwa ni ishara ya kutosha ya serikali kujali wananchi wake.” Amesema Rais Magufuli.