Home Mchanganyiko Tume ya Haki za Binadamu, Shirikianeni na TCRA Upatikanaji wa Haki za...

Tume ya Haki za Binadamu, Shirikianeni na TCRA Upatikanaji wa Haki za Mtandao-Waziri Kombo

0

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahamoud Thabit Kombo akizungumza katika kikao na ujumbe wa juu wa  watendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (kushoto), Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo(kulia), pamoja na waandishi wa habari katika ziara ya tume hiyo iliyofanyika Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahamoud Thabit Kombo( kulia) katika ziara ya tume hiyo iliyofanyika Zanzibar.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahamoud Thabit Kombo, akipokea mpango mkakati wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka  2018/2023 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu katika ziara ya uongozi wajuu wa tume iliyofanyika Zanzibar.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahamoud Thabit Kombo, akiwa kwenye picha ya pamoja ujumbe wa watendaji wa juu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora katika ziara ya tume hiyo iliyofanyika Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akizungumza na Waandishi (pichani), katika Ofisi za Habari, Utalii na Mambo ya Kale za Serikali ya Mapinduzi Zanzibarkatika ziara ya tume hiyo iliyofanyika Zanzibar.

………………………………………………………………………….

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mahamoud Thabit Kombo amesema kuwa tume ya haki za binadamu ina wajibu mkubwa wa kufanya kazi na wanahabari, pamoja na Mamlaka la Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kuwa sekta hizo ni kiungo muhimu katika utekelezaji wa haki za binadamu.

Akizungumza na ujumbe wajuu wa Tume hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti, Waziri Kombo alisema kuwa ugeni huo ni muhimu sana kwani habari huchochea upatikanaji wa haki za binadamu kwa kuibua mambo mbalimbali ambayo yako kinyume na haki za binadamu.

“Tume ya Haki za Binadamu wamekuja kututembelea sisi kwa sababu sekta ya habari ni kiungo kimoja wapo kikuu katika haki za binadamu na utawala bora kwa mujibu wa sheria na kanuni za haki za binadamu kimataifa na miongoni mwa mambo tuliyoyazungumza ni kusisitiza tume hii kututembelea mara kwa mara”, Waziri Kombo.

Alisema, kuwa mkutano wake na tume hiyo pamoja na waandishi wa habari ni faida kubwa kwa pande zote kwani utaleta kujifunza jinsi ya utekelezaji wa haki za binadamu ikiwemo upatikanaji wa habari kwa jamii ambayo nayo ni moja ya haki za binadamu duniani.

Alibainisha, kuwa tume hiyo inawajibu mkubwa wa kuona masuala ya haki za mtandao yanaenda vyema ili kuwezesha upatikanaji wa haki za binadamu kwa kila mtu kutumia mtandao kwa kuzingatia sheria na haki za kila mtu.

“Lakini pia tulizungumza masuala ya matumizi ya mtandao, kwa sababu kwa siku za karibuni masuala haya yanavunja haki za binadamu kwani watu wamekuwa wakitumia vibaya kutukana na kuwazalilisha wenzao hususani viongozi, hadi viongozi wajuu kabisa wanatukanwa lakini hakuna usimamizi wa haya mambo kwa hiyo tume mkifanya kazi pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), mtatusaidia upatikanaji wa haki kwenye masuala hayo”, Waziri Kombo.

Aidha, alisema kuwa masuala ya udhibiti wa redio, televisheni na magezeti uko vizuri ila masuala ya mtandao ndiyo yamekuwa ni magumu kidogo kwenye utekelezaji wa haki za binadamu kwani masuala haya yanatoa haki na uhuru wa kujieleza lakini uhuru huo umekuwa ukitumika vibaya kwa baadhi ya watu na kusababisha uvunjaji wa haki za binadamu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alibainisha lengo la ziara hiyo visiwani Zanzibari kuwa ni kuona jinsi gani tume hiyo inajijenga kwa kupata mahusiano mazuri kutoka kwa Serikali na Taasisi zake ili kuwezesha utekelezaji wa haki za binadamu kuwa rahisi.

“Lengo letu kubwa katika Wizara ya habari ni kujua utekelezaji wa haki za binadamu, tujue kwamba tunapozungumza haki za binadamu vilevile haki za watu kupata habari na haki za vyombo vya habari kutoa habari za utekelezaji wa haki za binadamu kwa uwazi zaidi”, Jaji Mstaafu Mwaimu.

Mwisho