Home Mchanganyiko SHULE ZOTE KUFUNGULIWA JUNI 29 MWAKA HUU NA SHUGHULI ZOTE KUENDELEA NCHINI

SHULE ZOTE KUFUNGULIWA JUNI 29 MWAKA HUU NA SHUGHULI ZOTE KUENDELEA NCHINI

0

…………………………………………………………….

Na. Alex Sonna, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi shule zote nchini kufunguliwa na shughuli zote nchini kuendelea kuanzia tarehe 29 Juni, 2020

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati wa kulihutubia bunge la jamhuri ya Muuungano wa Tanzania likihitimisha shughuli zake mwaka 2020.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa janga la Corona lipo na tutaishi nalo hivyo shughuli zote nchini ziendelea kufanyika kwa kufuata miongozo ya wataalamu wa afya juu ya kuchukua tahdadhali.

“29 Juni 2020 itakuwa jumatatu hivyo shule zote ziendelee na masomo na shughuli ziendele, tumewachelewesha watu kufunga ndoa ,” ameeleza Rais Magufuli