***************************
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Gerald Mweli amesema asilimi 90 ya wanafunzi wa kidato cha sita wameripoti shuleni katika halmashauri zote nchini.
Pia amsema mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kuwapo maambuziki ya ugonjwa wa Corona kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioripoti shuleni.
Akitoa tathimini ya uripotiji wa wanafunzi shule ambao walitakiwa kuanza masomo Juni 1 mwaka huu, Mweli alisema
Alisema wanafunzi hao wameanza masomo yao majuzi na kuwa leo wataanza kufanya mitihani ya majaribio ili kufanya tathimini ya maeneo ambayo wanafunzi yanawasumbua.
Aidha, Mweli alisema mpaka hakuna taarifa ya kuwapo mwanafunzi mwenye dalili za kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
“ Napenada niwatoe hofu wazazi kuwa watoto wanaafya njema na kuanzia jana na leo (juzi na jana) hatuna tukio au taarifa ya kuwapo mwanafunzi yeyote mwenye dalilia za kuwa ameambukizwa ugonjwa wa Corona.
Mweli pia alisema katika shule zote kumekuwapo maandalizi mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwa shule zote zimezingatia mwongozo uliotolewa na wizara ya afya.
“ Tumejipanga kuwa na maji ya kutosha, sabuni za kutosha katika shule zetu na kuzingatia suala la umbali wa mwanafunzi mmoja na mwingine ili kuwafanya wanafunzi wetu kuwa salama.”
Mweli aliongeza: “ Nimategemeo yetu kuwa ndani ya wiki mbili kutoka sasa wale wanafunzi ambao watakuwa wamefanya mitihani ya majaribio watakuwa wamesahihishiwa na kubaini maeneyo yenye upungufu
Alisema Tamisemi imeandaa program maalumu ya kuhakikisha topiki ambapo zimewatatizia wanafunzi zinafanyiwa marejeo
“ Nitoe wito kwa walimu na wakuu wa shule kuwa mipango tuliojiwekea na hali inavyokwenda sasa tuhakikishe tunasimamia na tunakuwa karibu na watoto na kuzungumza nao mara kwa mara na kuzidi kuwapa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Aidha, Mweli aliwataka walimu, wakuu wa shule na mameneja wa shule binafasi kuhakikisha wanatekeleza katazo la kuwataka wanafunzi kwenda shule na tangawizi, malimao.
“ Tulizuia wanafunzi kwenda na limao na tangawizi, hivyo hakuna sababu ya kuufanya mwanafunzi kushindwa kurudi shuleni kwa sababu hiyo.
“ Nitoe wito kwa walimu, wakuu wa shule na mameneja wa shule binafasi kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya serikali kuhuzu zuio la kuwataka wanafunzi kwenda na tangawizi, limao au spiriti ambayo yalikatazwa.
Aidha, Mweli alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamaia kwa karibu shule zilizo maeneleo yao ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama mpaka hapo watakapomaliza mitihani yao ya kidato cha sita.
Pia amwataka walimu, wakuu wa shule na mameneja wa shule binafsi wametakiwa kutekeleza mwongozo wa wizara ya afya uliotolewa na serikali na kuwa hawatasita kumchukulia hatua mtu yeyote anayekwenda kinyume na mwongozo na maelekezo ya shule.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alitangaza kufunguliwa kwa vyuo na wanafunzi wa kidato cha sita baada ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona kuzidi kupingua ikiwa imepita miezi kadhaa ya kufungua shule na vyuo kutokana na kuwapo kwa maambukizi ya ugonjwa huo.