Home Mchanganyiko CGP SULEIMAN MZEE APANDISHWA CHEO NA RAIS MAGUFULI TOKA BREGEDIA JENERALI...

CGP SULEIMAN MZEE APANDISHWA CHEO NA RAIS MAGUFULI TOKA BREGEDIA JENERALI KUWA MEJA JENERALI

0

Meja Jenerali Suleiman Mzee ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, akizungumza na Maafisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(hawapo pichani) mapema leo Juni 3, 2020 katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza leo Juni 3, 2020, jijini Dodoma. Meja Jenerali Mzee amepandishwa cheo hicho na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe Magufuli.

Meja Jenerali Suleiman Mzee ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza baada ya hafla fupi ya kumpongeza kupandishwa cheo kipya cha Meja Jenerali leo Juni 3, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza, jijini Dodoma

Mfungwa wa Gereza Kuu Isanga ambaye ni Kiongozi(Nyapara) akimpongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee kwa kupandishwa cheo kipya cha
Meja Jenerali.

Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo na Meja Jenerali Suleiman Mzee ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Magereza(hayupo pichani) leo Juni 3, 2020,jijini Dodoma.

Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee kwa kupandishwa cheo toka Bregedia Jenerali kuwa Meja Jenerali, leo katika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza.

(Picha zote na Jeshi la Magereza).