Mkuu wa Kitengo cha Biashara HaloPesa, Magesa Wandwi (Kulia), Akizungumza na waandishi kutoa ufafamnuzi huhusu HaloPesa gawio ambapo ni hatua ya kwanza kwa HaloPesa kutoa gawio kiasi cha shilingi bilioni moja kwa wateja wake Zaidi ya 1.9M ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala na washirika wake mbalimbali wanatumia huduma za HaloPesa.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara HaloPesa, Magesa Wandwi (Kulia), Akizungumza na waandishi kutoa ufafamnuzi kuhusu Halopesa Gawio ambapo Wateja wa HaloPesa watapata sehemu ya Gawio linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa Trust zilizoko katika mabenki mbalimbali nchini kati ya octoba 2016 na Disemba 2018.
……………………………………………………
Katika muendelezo wa kutoa huduma bora za kifedha nchini. Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel kupitia huduma zake za kifedha za HaloPesa, kufanya Gawio kwa wateja wake.
Hatua hii ikiwa ni hatua ya kwanza kwa HaloPesa kutoa gawio kiasi cha shilingi bilioni moja kwa wateja wake Zaidi ya 1.9M ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala na washirika wake mbalimbali wanatumia huduma za HaloPesa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha biashara cha HaloPesa Mr. Magesa Wandwialisema “Wateja watapata sehemu ya Gawio hili linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa Trust zilizoko katika mabenki mbalimbali nchini kati ya octoba 2016 na Disemba 2018.
Mr. Magesa Wandwi aliendelea kusema kuwa faida hiyo ni haki ya wateja na hivyo HaloPesa tunashauku na furaha kubwa ya kuwalipa wateja wetu gawio hilo kwa mujibu wa sheria ,kanuni na miongozo mbalimbali toka benki kuu ya Tanzania.
Gawio hili ni la kwanza kwa wateja wetu, na litatolewa ndani ya mwezi mmoja toka sasa, kiasi cha gawio ambacho mteja wa Halopesa atakipata anaweza kutumia atakavyo ikiwa ni pamoja na kutoa au kufanya miamala mbalimbali.
Tunapenda kuwasihi wateja wetu kuwa Halotel tunaendelea na tutaendelea kutoa huduma bora zenye gharama nafuu nchi nzima na waendelee kutumia huduma zetu za HaloPesa.