Home Mchanganyiko IGP SIRRO AWATAKA ASKARI POLISI KUFANYAKAZI KWA WELEDI

IGP SIRRO AWATAKA ASKARI POLISI KUFANYAKAZI KWA WELEDI

0

***************************

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari Polisi kote nchini kufanyakazi kwa kuzingatia weledi bila kumuonea mtu yeyote na kuendelea kuwachukulia hatua kali watu wanaojihusisha na uhalifu wa
kutumia silaha.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa mkoani Tabora ambapo alizungumza na Polisi Kata waliopo kwenye mkoa huo huku akiwataka kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake hasa tunapoelekea kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu sambamba na kuwachukulia hatua wale wasiotaka kufuata sheria.