Home Burudani AFISA UHUSIANO VETA AAMUA KUUWACHA UKAPELA

AFISA UHUSIANO VETA AAMUA KUUWACHA UKAPELA

0

**********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Jijini Dar es Salaam, Bw. David Edward Mpondyo  ameamua kufunga pingu za maisha na mkewe Bi. Vicky Philip Mgaiwa katika  Kanisa la waadventista Wasabato Ushindi Mikocheni, Jijini Dar es Salaam.

Kanisani watu wachache waliweza kufika kutokana na kuepuka mikusanyiko na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona.

Timu nzima ya Fullshangwe Media tunamtakia maisha mema yenye baraka tele katika ndoa yake na pia tutaendelea kushirikiana nae katika kazi pamoja na mambo mengine ya msingi.