Na Mwandishi Wetu
VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga kuna uwezekano mkubwa wakakutana tena kwa mara ya tatu msimu iwapo watavuka hatua ya Robo ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Hiyo ni baada ya ratiba ya Robo Fainali na Nusu Fainali ya michuano hiyo kupangwa leo katika studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo zilizopo Tabata Jijini Dar es Salaam.
Simba SC watakutana na mabingwa watetezi, Azam FC na Yanga SC watamenyana na Kagera Sugar katika Robo Fainali wote wakiwa nyumbani na vigogo hao wakishinda watakutana baina yao kwenye Nusu Fainali.

Robo Fainali nyingine zitakuwa ni kati ya Namungo FC dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na Sahare All Stars dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na washindi wa mechi hizo watakutana Nusu Fainali.
Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto aliyeongoza droo hiyo akisaidiwa na wachezaji wa zamani, beki wa zamani wa Simba SC Boniphace Pawasa na kiungo wa zamani wa Yanga, Deo Lucas amesema kuwa fainali itapigwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.
Mechi za michuano hiyo itapigwa kuanzia June 28,mwaka huu
.
.