Home Mchanganyiko KESI 42 ZA UDHALILISHAJI WANAWAKE NA WATOTO ZIMERIPOTIWA DAWATI LA JINSIA MKOA...

KESI 42 ZA UDHALILISHAJI WANAWAKE NA WATOTO ZIMERIPOTIWA DAWATI LA JINSIA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

0

Afisa-ustawi-wilaya-ya-kaskazini-A-Unguja-Khamis-Kona-akisisitiza-jambo

……………………………………………………………….

Na Masanja Mabula –Zanzibar.

JUMLA  ya kesi 42 za matukio ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto zimeripotiwa katika dawati la jinsia mkoa wa kaskazini Unguja kutoka mwezi Januari hadi mei mwaka 2020.

Akiwasilisha ripoti juu ya matukio hayo mkuu wa dawati la jinsia  mkoa wa kaskazini Unguja Fatma Juma Mahmoud alisema matukio hayo yamefanyika katika wilaya zote mbili za mkoa huo ambapo wilaya ya kaskazini A kumefanyika matukio 19 huku kaskazini B kumefanyika matukio 23.

Alisema  idadi kubwa ya kesi hizo  zipo katika hali ya upelelezi hadi sasa kwa lengo la kubaini ukweli juu ya watu wanaotuhimiwa kufanya matukio hayo.

Pia afisa huyo alisema kesi nyengine (2) hadi sasa zipo ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) zikisubiri kufikishwa Mahamakamani.

Kuhusu kesi ambayo ipo Mahakamani hadi sasa alisema ni kesi (1)Mahakamani moja na kwamba kesi hio imesita kuendelea kuskilizwa kwa kile alichokisema uwepo wa maaradhi ya korona ambapo Mahakama zimestisha shughuli za usikilizaji wa baadhi ya kesi.

Aidha  mkuu huyo wa dawati la jinsia alisema wamekua wakikabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo muhali kwa baadhi ya wanajamii jambo ambalo alisema linarudisha nyuma.

Kwa upande wake afisa dawati la jinsia wilaya ya kaskazini A Unguja Khamis Kona Khamis alisema kuendelea kuwepo kwa matukio hayo katika wilaya na mkoa huo kunachangiwa na sababu mbali mbali.

Akitaja baadhi ya sababu hizo alisema ni ucheleweshaji wa uandaaji wa kesi kabla kufikishwa Mahakamani.

‘’Mazingira ya aina hii hupelekea watu kukaa pembeni na kusuluhishana mwisho wa siku kesi haziendi Mahamani na hata zikienda hua hazina nguvu kwa kuwa wahusika hushindwa kutoa ushahidi’’aliongezea.

Hata hivyo alisema katika wilaya yake kumeibuka chanagmoto nyengine ya utekelezwaji wa watoto ambao wazazi huachana na kupelekea watoto kuhangaika hatimae kujikuta wamefanyiwa vitendo viovu.

Kwa upad wake mratibu wa dawati la jinsia katika mkoa huo Suleiman Juma alisema jeshi la polisi wanakabiliana na hali ngumu katika mapambano hayo.

Alisema kucheleweshwa kwa majalada ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka kunawapa mwanya mkubwa wahusika kukaa pemeni na kusuluhishana.

Alisema wakati wote huo hawawezi kukaa na mtuhumiwa ndani ya kituo cha polisi bali mtuhumiwa hutakiwa kuripoti kila baada ya muda lakini mara moja hupewa taarifa kuwa wahusika wameshaoana hivyo hawataki tena kesi.

Alieleza kuwa kwa mazingira hayo matendo ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto hayataweza kumalizika bila ya jamii kukubali kubadilika.

Meneja wa miradi kutoka Tamwa-Zanzibar Asha Abdi alisema jamii ina haja ya kubadilika na kurudi kwenye malezi ya zamani ikiwemo kuwaadhibu watoto wao pale wanapokosea.

Hata hivyo alisema kuna haja kubwa ya kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya sharia ambazo bado zinaonekana kuwa changamoto dhidi ya mapambano ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.