Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu na masuala mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa daftari la kudumu la Mipiga kura kulia ni Mkurugenzi wa Uchazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Mahera na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mbarouk S Mbarouk, Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Makamishna wa Tume ya Uchaguzi NEC kulia MH. Ramadhan Mapuri na kulia Jaji Thomas Mihayo wakiwa katika mkutano huo wa wadau wa Vyama vya Siasa.
Baadhi ya wadau kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakiwa katika mkutano huo.
Msajiri wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kulia akiwa katika mkutano huo pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndugu John Shibuda.
………………………………………………..
Wito umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage katika ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa kwa ajili kuweka wazi mabadiliko yaliyojitojeza kwenye Daftari la Awamu ya Pili ya Kupigia kura na kukabidhi nakala Kwa wawakilishi wa vyama vya siasa
Jaji Kaijage amesema Wananchi waliojiandikisha katika Daftari la wapiga kura Mwaka 2015 na wale waliojiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari Awamu ya kwanza wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao pindi Daftari litakapowekwa wazi katika maeneo yao na watumie njia nyingine za uhakiki Kama ilivyoelekezwa.
Jaji Kaijage amesema uboreshaji huo utaanza Aprili 17 na kukamilika Mei 4 mwaka huu kwa nchi nzima ambapo wamegawa katika ruti tatu na kufanyika kwa siku tatu kwa kila mkoa kwa Tanzania bara na Vusiwani.
Hata hivyo amesema kwa jumla ya vituo vitakavyotumika awamu hii ni 4006 badala ya 8031 vilivyokuwa vimekubaliwa hapo awali ambapo kwa sass vituo 3956 vitakuwa Tanzania bara na 50 Zanzibar.
Aidha amesema wananchi hususani wenye sifa ya kujiandikisha kama wapiga kura wapya wasisubiri kujitokeza siku ya mwisho ya zoezi na hivyo kusababisha msongamano bali wafike vituoni mara tu zoezi litakapowafikia na watuze kadi zao.
Aidha amesema uboreshaji huu utafanyika katika kila Kata ambapo kutakuwa na Mwandishi Msaidizi na BVR kit Operator ambao watakuwa na orodha ya vituo vyote katika Kata husika na watendaji hao watakuwa na uwezo wa kuboresha taarifa za mpiga kura yeyote.
Sambamba na hayo Jaji Kaijage amesema NEC haina wataalamu wa Afya ila imenunua vifaa vya kujikinga kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19 unaisababishwa na virusi vya corona na tayari wametoa maelekezo kwa watendaji wake kuzingatia miongozo ya wataalamu wa Afya.
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam leo.