Home Mchanganyiko SERIKALI KUJENGA ZAHANATI 3 KILA HALMASHAURI NCHINI

SERIKALI KUJENGA ZAHANATI 3 KILA HALMASHAURI NCHINI

0

Wazir wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba wakati  akiwasilishaji bajeti ya mwaka 2020/2021 ya wizara yake leo  jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imesema kila halmashauri itajengewa zahanati tatu kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu kwa wananchi wake.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Wazir wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati  akiwasilisha bajeti ya mwaka 2020/2021 ya wizara hiyo Jijini Dodoma.
 Mhe.Jafo amesema kuwa serikali itafanya Ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali 67 za halmashauri ili kuziwezesha kuweza kutoa huduma katika ubora unaohitajika.
Kwa upande mwingine amesema kuwa serikali inakamilisha ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa katika shule zote za halmashauri 184.
“Mhe.Naibu Spika serikali itajenga maabara saba katika kila halmashauri ili kuwezesha masomo ya sayansi kufundishwa katika ubora unao hitajika na kutoa wanafuzi wenye ujuzi unaohitajika,”amesema Mhe.Jafo.
Pia Mhe. Jafo amesema kuwa serikali inaendelea kusimamia shughuli za utawala bora na Kuratibu ujenzi wa miundombinu na shughuli katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili kuleta utendaji mzuri katika ofisi za serikali na wananchi kujifunia huduma zitolewazo na serikali yao.
Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa serikali itasimamia vyema Halmashauri 30 kuamia katika majengo yake ya utawala na Kutengeneza barabara zenye urefu wa kilomita zaidi ya elfu tatu katika miji na vijijini.