Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Dkt.Athuman Yussuf Ngenya akijibu baadhi ya changamoto zilizoibuliwa na wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha Mashauriano kati ya serikali na wafanyabiashara wa mkoa huo.
Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha wajasiriamali wadogo kufika TBS na kupata huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa bure bila malipo yoyote kwani shirika limetenga fedha kwa ajili ya kutoa huduma na wapo tayari kuwahudumia muda wowote.
Mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri nane (8) ,pamoja na wafanyabiashara zaidi ya 400 wa mkoa huo.