Home Mchanganyiko MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO ACHUKIZWA NA KUPIGA MARUFUKU KABISA ‘VIGODORO’ VYA...

MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO ACHUKIZWA NA KUPIGA MARUFUKU KABISA ‘VIGODORO’ VYA USIKU

0

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa akizungumza na wananchi wa Kata ya Nianjema kuhusiana na kupiga marufuku ngoma za usiku maarufu kama Vigodoro wakati wa Mkutano wake wa kikazi kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Baadhi ya Wananchi wa Wilayani Bagamoyo wakiwa wametulia kwa makini kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ambaye aliitisha Mkutano maalumu kwa ajili ya kuzungumzia mambo mbali mbali ya maendeleo kwa wakazi wa kata ya Njia njema pamoja na kuwasikiliza changamoto zao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

***************************

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ambaye pi ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amepiga marufuku kuwepo kwa ngoma  na miziki ambayo inafanyika nyakati za usiku bila utaratibu  maarufu kama ‘Vigodoro’ kwani zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili kwa wananchi.

Agizo hilo amelitoa  wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Nina njema, wadau wa maendeleo pamoja na wakuu mbali mbali wa idara wakati wa mkutano wake wa kikazi kwa ajili ya kusikiliza kero na changamoto mbali mbali za wananchi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuweka mipango  madhubuti kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo.

Zainabu alisema kwamba  katika baadhi ya maeneo ya Wilaya yake kumekuwepo  wimbi la ngoma ambazo zinachezwa nyakati za usiku na kupelekea kero na usumbufu mkubwa kwa watu wengine hivyo ameamua kuchukua hatua ya  kupiga marufuku hali hiyo kwa lengo la kuondokana na mambo mbali mbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hasa katika wakati wa usiku.

“Kuanzia leo katika mkutano huu napenda kusema napiga marufuku kabisa mambo ya vigodoro vya usiku kwani vimekuwa ni kero sana na vinachangia kwa kiasi kikubwa katika kunjunja maadili ya Mtanzania na kwamba katika hili nitahakikisha ninalisimamia kwa ukaribu mno ili kukomesha kabisa kuwepo kwa hali hii kayika Wilaya ya Bagamoyo,”alifafanua Zainabu.

Aidha Mkuu huyo alibainisha kwamba wananchi wa Bagamoyo kwa sasa wanatakiwa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za miradi ya maendeleo kuliko kutumia muda wao mwingi katika kukesha nyakati za usiku wakicheza ngoma ambazo hazina faida yoyote katika Taifa la Tanzania.

“Mimi kikubwa ninachotaka kuwaambia hasa wananchi wa Wilaya ya Bgamoyo tuachane kabisa na kujikta zaidi katika kukesha kwenye vigodoro. kabisa  ni vema zaidi mkatumia fursa mbali mali zilizopo mkajishughulisha katika shughuli za kujipatia kipato ili kuweza kuondokana na  wimbi la umasikini hivyo ni rai yangu wote tukashirikiana katika kuleta maendeleo na sio kukesha kwenye vigodoro ambavyo ni havina faina yoyote ile,”alisema Zainabu.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya alifafanua kwamba mtu yoyote ambaye anahitaji kufanya shughuli yake ya usiku ni lazima apatiwe kibali maalumu kutoka katika Ofisi yake kwa kuzingatia sheria na utaratibu ambao utakuwa umewekwa,ili kuhakikisha mambo yote ambayo yanakuwa yanajitokeza nyakati za usiku ikiwemo masuala ya  uharifu  na wizi yanakomeshwa kwa kiasi kikubwa.

Katika  hatua nyingine ametoa onyo kali kwa wale wote ambao watabainika kukiuka agizo lake ambalo amelitoa na kwamba atahakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria wale wote ambao watabainika bado wanaendeleo kinyemela  kujihusisha na  masuala ya kupiga ngoma za usiku na vigodoro bila ya kuwa na kibali maalumu.

Nao baaadhi ya wananchi ambao hawakuta kutaja majina yao walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa hatua ambayo ameifanya ya kupiga marufuku kabisa mambo ya vigodoro hasa katika nyakati za usiku kwani yamekuwa ni tatizo kubwa kutokana na kuwepo kwa matukio mbali mbali ambayo yanasabisha momonyoko wa maadili hasa kwa vijana.

“Kwa kweli sisi kama wananchi wa Wilaya ya Bgamoyo hili agizo la Mkuu wetu kupiga marufuku ngoma za usiku maarufu vigodoro sisi tunamuunga mkono kwa asilimia mia moja kwani imekuwa ni kero sugu ya siku nyingi na wakati mwingine yani watu hatulali kabisa na kingine kuna baadhi ya matukio ambayo yanafanyika hivyo kwa hatua hii itaweza kusaidia kuondoa na kupunguza kabisa changamoto amabzo zimekuwa zikijitokeza katika maeneo ambayo tunaishi,”walisema.

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa maendeleo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nianjema Abdul Pyalla alisema kwamba suala hilo la vigodoro  ni kweli limekuwa ni kero kubwa kwa wananchi hivyo atahakikisha kushirikiana bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya  pamoja na wananchi husika katika mitaa mbali mabli kwa lengo la kuwaelimisha zaidi kuhusu umuhimu wa kutumia muda wao katika shughuli za maendeleo kuliko kukesha kwenye ngoma.