Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiendelea na ziara yake ya siku tatu Mkoani Mtwara, Mbunge wa Tandahimba Ndg. Katan Ahmed Katan amejivua uanachama wa CUF na kujiunga na CCM hapo jana.
Mbunge huyo wa Tandahimba, amejiunga na CCM jana tarehe 21 Februari, 2020 katika mkutano wa ndani uliokuwa ukiendelea katika jimbo la Nanyamba Mtwara vijijini, ambapo amepokelewa na Katibu Mkuu kwa niaba ya wanachama wote wa CCM.
Katibu Mkuu akifafanua kabla ya kumpokea Mbunge huyo, amesema
“Nilipokuwa naawambia nafunga mitambo walidhani ni utani, sasa nataka kuwathibitishia hapahapa leo, kwa kumpokea Mbunge mwingine na bado watakuja wengine wengi.”
Katibu Mkuu yupo Mkoani Mtwara kwa Ziara ya kikazi ya siku tatu ya kuimarisha Chama na kuendelea kukirejesha Chama kwa wanachama.