Na Magreth Mbinga
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeongeza muda wa siku Tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Mkoa wa Dar es saalam na zoezi hilo litakamilika February 23 mwaka huu
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Uchaguzi TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WILSON MAHERA amesema kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu Cha 15(1) Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 243 na kifungu Cha 21(1)Cha Sheria ya Uchaguzi wa serikali za mitaa sura 292 tume imeamua kuongeza muda huo ili kusaidia baadhi ya Wananchi kujiandikisha ili washiriki haki yao ya msingi kuwachagua viongozi wanaowataka
“Tumeamua kuongeza muda kwasababu siku ya Jana Watu wengi walijitokeza kujiandikisha nawasihi wananchi watumie siku hizi Tatu kwa ajili ya kujiandikisha kwa awamu hii ya kwanza ya zoezi la uboreshaji wa daftari la Kudumu “.
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa katika muda huo wa nyongeza vituo vyote vya uandikishaji vitaendelea kufunguliwa saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni hivyo wananchi ambao Bado hawajajiandikisha na waliopoteza kadi zao za kupigia kura wafike vituoni wakahudumiwe.
Aidha tume inaendelea kuwasihi wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kutumia muda huo vizuri ulioongezwa kuhakikisha taarifa zao zinaingizwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka na kuchaguliwaTU.