Home Mchanganyiko TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea
kuwa salama na mali zao.

 

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea
kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu
pamoja na ajali za barabarani.

 

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO KUWA ZA WIZI.

 

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia kijana DAVID MUSA [20] Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya kwa tuhuma ya kupatikana na mali zidhaniwazo kuwa za wizi.

 

Tukio hilo limetokea tarehe 18.02.2020 majira ya saa 16:10 jioni huko Mtaa wa Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika msako uliofanywa na
Jeshi la Polisi mkoani hapa na kumkuta mtuhumiwa akiwa na Kamera moja [01] aina ya Cannon 7D, Lens mbili [02] ndogo aina ya Canon 7D, simu ndogo nne [04] aina ya
Tecno mbili, Itel moja na Samsung moja na laini tatu [03] za Tigo, Vodacom na Halotel mali zidhaniwazo kuwa za wizi.

 

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

 

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI TOKA NDANI YA GARI.

 

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa watano 1. JOSEPH MOHAMED [38] Mkazi wa Airport ya Zamani, 2. PASCHAL JOHN [57] Dereva Hiace na Mkazi wa Mwambene, 3. MAWAZO SAMWEL [28] Dereva na Mkazi wa
Mafiati, 4. IBRAHIM MAKOKULA [25] Mkazi wa Ilomba na 5. ZAWADI RICHARD [25] Mkazi wa Makunguru kwa tuhuma za wizi toka ndani ya gari.

 

Tukio hili limetokea tarehe 15.02.2020 majira ya saa 11:00 asubuhi huko Stendi ya Mabasi Nanenane Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kupata taarifa
za kuwepo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya wizi toka ndani ya magari hasa kwa abiria ndipo ulifanyika msako kwa kushirikiana na viongozi wa Stendi ya Mabasi
Nanenane na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kuhusiana na matukio hayo.

 

Aidha katika msako huo, yamekamatwa magari mawili yenye namba za usajili T.632 BQQ aina ya Toyota Hiace na T.780 CZT aina ya Toyota Hiace ambayo hufanya
safari kati ya Stendi Kuu – Uyole ambayo yanatuhumiwa kwamba vitendo vya wezi kwa abiria hutokea.

 

Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa watuhumiwa wengine pamoja na gari moja ambalo limetajwa kuhusika katika matukio hayo.

 

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI.

 

Jeshi la polisi mkoani mbeya linawashikiliae watuhumiwa wanne [04] 1. MASIKITIKO PATSON @ MBUZI [34] Mkazi wa Mtakuja 2. HURUMA MWASILE [36] 3. AMANI MSWIMA [21] Mkazi wa Mlima reli na 4. EZEKIA SINKALA [26] Mkazi wa Mtakuja kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio ya
unyang’anyi, uporaji wa Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya.

 

Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 12/02/2020 baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanyika msako maalum maeneo mbalimbali ya Mbalizi na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao. Watuhumiwa wote wamehojiwa na kukiri kutenda matukio mbalimbali kama ifuatavyo:-

 

1. Mnamo tarehe 20/12/2019 majira ya usiku huko Mtakuja mtu aitwaye ZACHARIA JACKSON [30] dereva bodaboda aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyang’anywa pikipiki yake aina ya T- BETTER
yenye namba za usajili MC 149 CFJ.

 

2. Mnamo tarehe 10/02/2020 huko MtakujaUtengule Usongwe mtu aitwaye SHUKURU JUMA [26] aliuawa kisha kunyang’anywa pikipiki yake aina
King lion.

 

3. Mnamo tarehe 29/01/2020 huko ZZK Mbalizi majira ya usiku mtu aitwaye SADOCK NIMROD [21] dereva bodaboda alivamiwa na kisha kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kisha kunyang’anywa Pikipiki.

 

 

Upelelezi wa mashauri haya unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WAHALIFU SUGU WA MATUKIO YA UVUNJAJI.

 

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili 1 .MAJALIWA CHARLES [18] Mkazi wa DDC Mbalizi na 2. ANDWELE ANDIGENIE MWAKAOISON [26] Mkazi wa DDC.

 

Tukio hili limetokea mnamo tarehe 19/02/2020 majira ya saa 17:00 alfajiri katika msako maalumu uliofanyika huko maeneo ya DDC Mbalizi, Kata na Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa na baada ya kuwapekua wamekutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-

 

1. Televisheni mbili inchi 52 aina ya hitech na inchi 32 aina ya samsung
2. CPU mbili aina ya dell
3. Monitor mbili [2] aina ya samsung na dell
4. Laptop moja aina ya hp
Watuhumiwa wamekiri kuhusika kwenye matukio ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.
baadhi ya mali zimetambuliwa na wahusika.