Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa UTT
AMIS, Simon Migangala.
****************************
Na Mwandishi Wetu
UTAJIRI sio fedha ambazo mtu anakusanya bali ni fedha
zinazowekwa na kufanya kazi. Tamaduni zetu zimeifanya jamii kubwa kuhifadhi fedha ndani katika vyungu, magodoro, vibubu.
Uwekaji akiba na uwekezaji ni dhana mbili tofauti. Uwekaji
akiba ni mzuri lakini bila kuziwekeza ni bure. Ili uwe muwekaji akiba mzuri, unapaswa kuwa na nidhamu ya kujizoesha muda mrefu.
Nchini Tanzania unaweza kuwekeza fedha zako katika masoko ya fedha, mitaji. Hatua hiyo inahusisha akaunti za muda maalum na zisizo za muda maalum katika benki za biashara.
Pia hati fungani za Serikali za muda mfupi, mrefu, kampuni na
hisa zilizoorodhoshwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE)
zina nafasi kubwa ya kurejesha gawio zuri.
Uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko ambayo
wanaisimamia ni fursa mbadala inayowezesha watu, vikundi, taasisi, kampuni kuwekeza pesa zao kwa
Meneja wa UTT.
Meneja huzichukua fedha hizo, kuziwekeza kwenye masoko ya fedha, mitaji kulingana na waraka wa
makubaliano. Faida ambayo hupatikana hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa
uwekezaji uliofanyika kwenye mfuko husika.
Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja UTT AMIS (UTT Asset Management and Investor Services) ni ya
serekali iliyo chini ya Wizara ya Fedha, Mipango ikisimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana Tanzania (CMSA).
Msingi wa kampuni hiyo unatokana na Unit Trust of Tanzania (Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ambayo
ilianzishwa mwaka 2003 na kuanza rasmi kazi ya kubuni, kuendeleza Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja
mwaka 2005.
Mwaka 2013 UTT ilibadili jina na kuitwa UTT AMIS, jukumu la kampuni ni kubuni, kusimamia na
kuendeleza mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini.
Hadi sasa kuna mifuko sita ya uwekezaji ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Kujikimu, Ukwasi,
Mfuko wa Hati Fungani (Bond Fund) pamoja na huduma maalumu ya usimamizi wa mali (fedha) kwa
wateja wenye fedha
kuanzia sh. milioni 100 lakini wasingependa kuwa chini ya mifuko.
UTT AMIS inasimamia zaidi ya sh. bilioni 337 kwa ujumala. Mfuko wa Umoja ndiyo mkubwa kuliko yote
ukiwa na zaidi ya bilioni 219, Mfuko wa Wekeza Maisha sh. bilioni 1.1, Watoto
sh. bilioni 3.2. Kujikimu sh. bilioni 18, Ukwasi sh. bilioni 73, Bond sh. bilioni 29, Huduma maalumu kwa
wateja zaidi ya sh. bilioni 12.
Bei ya kipande kwa kila mfuko imekuwa kwa wastani mzuri sana Umoja ni kuanzia sh.70 hadi sasa zaidi
ya sh. 610, Wekeza kuanzia sh. 100 hadi zaidi ya sh. 430, Watoto kuanzia sh. 100 hadi zaidi ya sh. 357,
Jikimu zaidi ya sh. 129, Ukwasi kuanzia sh. 100 hadi zaidi ya sh. 231, Bond kuanzia sh. 100 hadi zaidi y
ash. 103.
Mfuko wa Umoja ulianza mwaka 2005, hadi sasa umekua zaidi ya mara 8.7. Kila aliyeweka pesa wakati
mfuko unaanza pesa zake zimekuwa mara 8.7.
Uzuri wa Mfuko huu ni rahisi kujiunga, kianzio cha kuwekeza ni vipande 10 tu, bei ya kipande kwa sasa
sh. 610 hivyo anzia sh. 6100 tayari unakuwa mwekezaji. Unaweza kuwekeza katika mfuko huu kwa njia
ya simu.
Hakuna kikomo cha juu cha kuwekeza, ukuwaji wake ni mzuri tofauti na pesa yako kama ungeiwekeza
mahali pengine kama kwenye baadhi ya hisa, benki, hati fungani hasa za muda mfupi.
Faida nyingine ni wepesi wa kupata pesa zako unapozihitaji, kuongeza pesa ndani ya uwekezaji, kama
unahitaji sehemu tu ya pesa zako, kujua thamani ya uwekezaji wako kila siku na unafuu wa miamala.
Wekeza Maisha ulianzishwa mwaka 2007 na umekuwa mara 4.3 ambapo pamoja na ukuwaji huu, mfuko
huo umekuwa ukitoa faida pacha, kukuza mtaji na bima dhidi ya kifo, ulemavu na gharama za mazishi.
Pia mfuko umekuwa ukikuwa zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka na kiasi kinachokatwa kwa ajili ya bima ni
chini ya asilimia moja hivyo ni kama umepata bima bure.
Kumbuka bima nyingi zina kikomo cha mwaka lakini Wekeza Maisha ni mpango wa miaka kumi, kiasi
cha bima ni kuanzia sh. milioni moja hadi sh. milioni milioni 25, chaguo ni lako.
Unaweza kuchukua pesa zako hadi asilimia 75 baada ya miaka 5, Mfuko unajumuisha hisa, akaunti za
muda mfupi na hati fungani za muda mfupi na mrefu hivyo kukupa nafasi ya kuvuna faida nzuri sana
pale hisa zinapokua zimekuwa vizuri.
Mfuko wa Watoto ulianzishwa mwaka 2008, hadi sasa umekuwa zaidi ya mara 3.5. Hii ina maana kuwa
kwa aliyekuwa amewekeza sh. milioni 10, sasa ana sh. milioni 35.
Hiyo ni faida nzuri sana, mtoto kuanzia kuzaliwa hadi miaka 18 atakuwa mwekezaji katika mfuko huu na
bado anaweza kuacha uwekezaji ndani ya mfuko hadi miaka 24.
Mtoto aliye chini ya miaka 24 haruhusiwi kuingia mikataba ya kisheria hivyo mzazi atakuwa mwangalize.
Si lazima uwe na sh. milioni 10 kama mfano unavyoelekeza. Unaweza kuanza kuwekeza sh. 10,000 tu.
Wekeza mara nyingi jinsi uwezavyo.
Mfuko wa Jikimu una lengo la kukidhi mahitaji ya wawekezaji
wanaohitaji uhakika wa mapato ya mara kwa mara.
Ulianzishwa Novemba 3, 2008, unatoa gawio mara nne kwa mwaka kwa yeyeto mwenye zaidi ya sh.
milioni 2, gawio mara nyingi limekuwa kati ya sh. 2.5 hadi sh. 4, kiasi cha faida kikiwa zaidi ya hapo kina
jumuishwa kwenye kiasi cha msingi kilichowekezwa.
Kwa mwenye sh. milioni moja hadi chini ya sh. milioni 2 gawiwo ni mara moja kwa mwaka. Ki-asilimia
gawiwo limekuwa kati asilimia 2.5 hadi asilimia 4 ambapo kwa mwaka inakuwa kati ya asilimia 10 hadi
16.
Kama faida ilizidi hizo asilimia itaongzwa kwenye mtaji. Mfuko hauna kiwango cha juu cha kuwekeza ,
mwekezaji anaweza wekeza mara nyingi awezavyo.
Mfuko wa Ukwasi umekuwa zaidi ya mara 2.3 ndani ya miaka 5, hii ina maana kuwa, kama uliwekeza sh.
milioni 10 sasa una sh. milioni 23, kama sh. milioni 100 sasa una sh. milioni 230.
Hiyo ni faida nzuri sana, si laizma uwe na mamilioni, unaweza kuanza kuwekeza kidogo kidogo kuanzia
sh. 100,000 na ukawa unaongeza kiasi cha sh. 10,000 kila unapopata si lazima kila mwezi.
Mfuko huu umezingatia athari za uwekezaji wa kina, ukuaji wake umekuwa ni wa wastani mzuri sana na
hakika mfuko una ukwasi wa hali ya juu yaani wepesi si wa kufanya miamala bali ni pamoja na muda
mfupi wa kupata pesa zako baada ya kuuza vipande.
Mfuko mpya wa Hati Fungani unaojulikana kama ‘Bond Fund’ ni kati ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja
inayoendeshwa na UTT AMIS ulioanzishwa kwa malengo maalum.
Mfuko huo una miezi 5 tangu kuanzishwa na umeshatoa gawiwo la kwanza, ndani ya muda huo
mchache, bei ya kipande ilianzia shilingi sh. 100 na sasa ni sh. 103.8, hiyo ni faida nzuri.
Kuanzishwa kwa Mfuko wa Hati Fungani kumetokana na mahitaji ya wawekezaji kutaka bidhaa zenye
tija zaidi na utafiti wa kina na wakitaalamu.
Mfuko unawawezesha wawekezaji wadogo na wa kati kuzifikia fursa za uwekezaji ambazo kwa hali ya
kawaida ni wawekezaji wachache na wakubwa ndio wange zifikia.
Kupitia mfuko huu utapata faida kushiriki kwa namna moja au nyingine kwenye uwekezaji katika hati
fungani za muda mrefu na muda mfupi kwa asilimia 90, asilimia 10 itakuwa kwenye uwekezaji wenye
ukwasi mkubwa mfano hati fungani za muda mfupi na akaunti za benki za muda mfupi.
Lengo la kuwekeza asilimia 10 kwenye bidhaa zenye ukwasi mkubwa ni kuwawezesha wawekezaji
wanaohitaji kuchukua fedha kutoka kwenye uwekezaji wao katika mfuko wafanye hivyo kwa haraka na
wepesi.
Mfuko umeundwa ili kumwezesha kila mwekezaji kuchagua kama anapenda kukuza mtaji au kupokea
gawiwo kwa mwezi, kila miezi sita kutokana na mahitaji yake ya kifedha.
Akiuzungumzia mfuko huo, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, alisema
umelenga kuondoa changamoto za kipato cha kila mwezi, au miezi sita au kukuza mtaji.
Anaongeza kuwa, baadhi ya wawekezaji hasa wadogo ni vigumu kuwekeza kwenye baadhi ya bidhaa
katika soko la fedha ila kupitia mfuko wa Hati Fungani unawawezesha kufanya hivyo.
Mwekezaji anapata faida sawa na wawekezaji wakubwa, akihitaji fedha anauza baadhi ya umiliki wake
kwenye mfuko kwa utaratibu rahisi bila kupoteza faida aliyoipata.
Pia mfuko huo unawafaa wawekezaji wakubwa kwa sababu ya faida shindani, gharama ndogo za
kuwekeza, ukwasi wa kutosha, usalama wa mtaji, hatari ndogo za uwekezaji.
Mfuko unatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza, kushiriki katika masoko ya mitaji, kufaidika na uwekezaji
huo.
Kwa mantiki hiyo, mfuko umeandaliwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa kipato cha chini, kati na kipato
cha juu ambao ni watu binafsi, kampuni, taasisi na vikundi rasmi wanaweza kushiriki katika uwekezaji
kwenye mfuko huo.
Mbaga anasema, mfuko una mipango miwili ya uwekezaji ili kukidhi matakwa tofauti ya wawekezaji.
Kuna mpango wa kukuza mtaji, gawio kila mwezi, gawio kila miezi sita, mpango wa kukuza mtaji.
Gawio la mara kwa mara halitatolewa kwa wawekezaji badala yake faida iliyopatikana itarudishwa
kwenye uwekezaji wa awali kwa kununua vipande vitakavyonunuliwa kwa bei ya wakati huo.
Mpango huo utawafaa wawekezaji wanaohitaji kuweka akiba kwa malengo maalum mfano kujenga
nyumba au wafanyakazi wenye kipato kama wangependa kuwa na fedha ya akiba.
Wawekezaji katika mpango huo wanaweza kuuza kiasi chochote cha uwekezaji kama wamekidhi vigezo
vinavyohusu uuzwaji wa vipande.
Pia wawekezaji wanaohitaji kuchukua faida kila mwezi kama wastaafu wanaopata fedha zao za mkupuo,
kuwekeza kwenye mfuko, wanashauriwa kuchagua kupokea gawio kila mwezi ili wapate kipato cha
kuishi bila kupoteza fedha walizopata.
Mbaga anasema wawekezaji wengine wanaopata fedha nyingi mara moja mfano wachimba madini,
wanaweza kuchagua gawio kila mwezi ili wafanye shughuli zao bila kuathiri mtaji wao.
Pia wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vyote ili mradi wawe
wamekidhi vigezo vya mfuko vinavyohusu uuzwaji vipande.
Kuhusu mpango wa gawio kila miezi sita, Mbaga alisema hutegemea na mahitaji ya fedha ya mwekezaji
na anavyochagua kwenye fomu ya maombi ya kuwekeza kwenye mfuko.
Kwa wawekezaji ambao wanahitaji kuchukua faida kila miezi sita mfano wafanyakazi wanaohitaji
kuweka kiasi cha fedha ili faida inayopatikana itumike kulipa ada kusomesha watoto, wanaweza
kuchagua kupokea gawio kila miezi sita.
Pia kuna wawekezaji wanaopata fedha nyingi mara moja kama wakulima wa mazao mbalimbali ya
msimu, wanaweza kuchagua kupata gawio kila miezi sita.
Wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza kuuza vipande kidogo au vipande vyote ili mradi
wawe wamekidhi vigezo vya mfuko.
Kwa kifupi, uwekezaji wa pamoja ni uwekezaji ambao umaarufu wake unazidi kukuwa kila siku duniani,
unazingatia misingi au taratibu maalumu kama ilivyoainishwa ndani ya waraka wa makubaliano.
Pia makubaliano huzingatia taratibu za uwekezaji za kila siku, thamani ya mwanzo ya kipande, maeneo
ya kuwekeza, misingi mingine mbalimbali.
Jambo la msingi ni jinsi hali hatarishi katika uwekezaji
zitakavyokabiliwa hasa ikizangatiwa kuwa, lengo kuu ni kupata faida hivyo viashiria vya hatari katika
uwekezaji vikizingatiwa kipande au thamani ya pesa katika uwekezaji inaweza kupanda au kushuka.
Uwezekano wa kupata hasara hupunguzwa kwa kutawanya sehemeu za kuwekeza. Mfano kwenye hisa
na kwenye masoko ya fedha. Sehemu hizi mbili pekee ni dunia ya uwekezaji, hakuna sababu ya kuweka
mayayi yote katika kapu moja.
Hasara pia inapunguzwa na Meneja wa Fedha zilizo kwenye uwekezaji wa pamoja lazima awe mtaalamu
mbobezi, leo hii Watanzania wengi bado wanajiuliza kipande ni nini? Hisa ni nini? Akaunti ya muda
maalumu ni nini na hati fungani ni nini?
Maswali haya na jinsi ya kushiri katika uwekezaji huu ambao misingi yake ni faida, athari za uwekezaji
zikiwa
zimezingatiwa na kusimamiwa yanajibiwa na wataalamu kama madalali wa soko la hisa vitengo vya
uwekezeji katika benki, kampuni kama UTT AMIS.
Faida kubwa nyingine haijalishi kipato, mwenye kipato kikubwa na kidogo wote wanapata faida sawa
kwa kipande ila mwenye vipande vingi atavuna zaidi.
Cha msingi ni kwamba, mwenye sh. 10,000 anaweza kuwa mwekezaji na anaweza kuwekeza mara nyingi
anavyoweza bila kujali muda.
Kwa wewe mwenye biashara na unapata faida kila siku unaweza kukusanya faida na kuiwekeza kila siku
au ukakusanya na ukaweka japo mkupuo mmoja kila wiki hivyo ukaipa faida.
Jambo la muhimu ni muda, uwekezaji ni jambo linalohitaji muda ili kukabiliana na mawimbi ya kupanda,
kushuka kwa thamani. Ni kama mti ukipanda mbegu inaanza mizizi inaenda chini, halafu mmea unaota
na baadae mti wenye majani, maua na hatimae matunda.
Gharama za uwekezaji zinapunguwa sana tukiwekeza pamoja, sote tunajuwa tunalipa nauli kubwa sana
kama tukisafiri peke yetu kwa teksi kuliko tukisafiri pamoja kwa daladala.
Pia tunapata punguzo dogo sana tukijadili bei kwa bidhaa chache kuliko tunapojadili manunuzi ya bidhaa
nyingi.
Kilo moja inapunguza aslimia 2 lakini kuanzia kilo 10 na kuendelea asilimia 4 hivyo pesa zikiwa nyingi
zinaongeza nguvu ya majadiliano.
Pia pesa zikiwa nyingi zinakupa nafasi yakufanya uwekezaji ambao peke yako usingeweza kwa pesa
chache mfano hati fungani, hisa na akaunti za muda maalumu ni vitu vinavyohitaji kuanzia kiasi fulani
cha fedha.
Faida nyingine ni unafuu katika kodi, serikali na si Tanzania tu bali kote duniani waliamua kwa makusudi
kuweka kiasi kidogo cha kodi katika mfumo wa uwekezaji ili kumpa unafuu mwekezaji.
Zaidi ya hapo mwekezaji anapewa fursa ya kuchaguwa mfuko kutokana na malengo yake. Mfano Mfuko
wa Umoja hukuza mtaji, Jikimu-gawiwo mara nne kwa mwaka, Watoto- elimu na maisha baada ya
kufuzu, Ukwasi-kipato cha muda mfupi wa kati na mrefu.
Pamoja na faida za uwekezaji wa pamoja changamoto pia zipo kwa mfano, wawekezaji wanampa fedha
Meneja ambaye naye anaziwekeza kwa niaba yao.
Meneja anatakiwa awe amebobea, awe na ufanisi wa hali ya juu, awe mkweli na mwenye kufuata
masharti ya uwekezaji kwa mfano, Kampuni ya UTT AMIS ni ya serekali, imekuwepo kuanzia mwaka
2003 na kuanzisha uwekezaji wa pamoja mwaka 2005 ambapo kwa kipindi chote imekuwa ikifanya vizuri
sana.
Changamoto nyigine katika uwekezaji, kumbuka kuwa moja wapo ya sehemu fedha zinawekezwa
kwenye hisa, hisa zinapanda na kushuka, hisa ni kioo cha vipande kwa mifuko yenye asilimia fulani ya
hisa katika uwekezaji wake.
Hisa zikishuka thamani ya mfuko inashuka pia, thamani ikishuka mwekezaji na Meneja wanapata kidogo
hivyo Meneja lazima awe makini kwenye kuchagu hisa zipi anunue.
Kwa kawaida serikali au mtu binafsi ndiye mwanzilishi, halafu fedha zitakazowekezwa zitatoka kwa
wawekezaji, mwanzilishi atapata faida na mara nyingi haifiki hata zaidi ya asilimia 2 ya thamani ya kiasi
kilichowekezwa.
Jitahada na juhudi za kuwashawishi wawekezaji kuwa kila jambo litakuwa sawa zinahusika pale mwanzo
kadri uwekezaji unavyosogea mbele hivyo lazima kutoa taarifa sahihi za ukuwaji wa uwekezaji ili kuvutia
wawekezaji.
Wawekezaji wakiwa wengi fedha zitakuwa nyingi na kufidia gharama za lazima, gharama zingine za
uendeshaji. Kama kuna madeni lazima uwiano kati ya mtaji na madeni uwe mzuri.
Changamoto nyingine ni kuna kufilisika, hii inaweza kusababisha kutoa mali zote zilizo wekezwa na
inawezekana kukawa bado kuna uwekezaji ambao ulikuwa bado haujawiva.
UTT AMIS inasimamia sh. bilioni 280 na kila siku inazidi kupanuka. Muda wa kwanza wa kuwekeza
ukiisha inabidi uwekezaji uendeleee, pengenine riba kwa wakati huo zinakuwa zimeshuka katika soko la
awali au soko la pili.
Changamoto zingine ni kupungua kwa thamani ya fedha, mfumuko wa bei pamoja na nyinginezo.
Changamoto nyingi zikiwemo mabadiliko katika sera za uwekezaji, hali ya uchumi wa nchi, kutoa fedha
katika uwekezaji wa muda mrefu ili kuwekeza katika muda mfupi au muda mfupi kwenda muda mrefu.
Ili kukabiliana na changamoto, mwekezaji katika Kampuni ya UTT AMIS lazima ajuwe kuwe kampuni hii
ni ya serekali na imeanzishwa kufuata taratibu za kisheria.
Kampuni iko chini ya Wizara ya Fedha, pia kuna kampuni nyingine binafsi za namna hiyo. Mfano lazima
kuwe na mwangalizi wa fedha/mali ambapo kwa UTT ni benki ya CRDB.
Lazima kuwe na wakaguzi wa ndani na nje wa hesabu, Mkaguzi Mkuu wa Serikali na KPMG ili hufanya
kazi hiyo, kuna waraka wa makubaliano ambo unaainisha taratibu mbalimbali za lazima.
Kila mfuko una kitabu chake chenye kuonyesha tabia za mfuko na kanuni mbalimbali, licha ya hivyo
wawekezaji wana nafasi ya kuchangia mabadiliko kwenye Mkutano Mkuu wa wakezaji wa mwaka, pia
wanaweza kumkataa Meneja kama wanaona hafai.
Hakuna ukomo wa kununua vipande, kwa kutumia simu unaweza nunua kila siku hata saa ambazo si za
kazi yaani saa 24.
Watanzania wengi wanadhani kuwa, unawekeza mara moja tu basi halafu unasubiri, tukifikiri hivyo
tutakuwa tunakosea, wekeza mara nyingi unavyoweza na jaribu kuwa na subra ili kuupa uwekezaji wako
muda wa kukuwa.
Kumbuka kiasi cha chini ni sh. 10,000 kwa kila mfuko isipokuwa Mfuko wa Ukwasi ambao unaanzia sh.
milioni 100,000 na Mfuko wa Hati Fungani sh. 50,000 huku nyongeza ikiwa kuanzia sh. 10,000 kwa
ukwasi na sh. 5,000 kwa Mfuko wa hati fungani.
Kumbuka tofauti na hisa, kipande unauza na kunua wakati wowote hivyo huhitaji kusubiri kupata pesa
zako, ndani ya siku kumi utakuwa umepata pesa zako katika akaunti yako uliyoainisha, kama ilivyo kwa
binadamu, ukifariki mrithi uliyemwandika katika fomu za kujiunga ndiye
atakayesimamia uwekezaji wako.
Pesa zinazopatika kutoka katika uwekezaji zinagawiwa kwa kila
mwekezaji kwa asilimia sawa kutokana na idadi ya vipande vyake.
Baadhi ya mifuko mwekezaji atapata gawiwo katika kila kipindi cha muda fulani, mwekezaji anaweza
kuacha gawiwo hilo katika uwekezaji, baadhi ya mifuko mwekezaji atachukua faida yake pale
anapohitaji, pia mwekezajia anaweza kutoka katika uwekezaji wakati wowote.
Uwekezaji wa pamoja unaweza kuwa anuwai yaani mseto, pia mfuko unaweza ukawa unawekeza
kwenye hisa tu, yaani kwenye kampuni zilizo orodhozeshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam.
Kwa Tanzania hatuna mfuko unaowekeza kwenye soko la hisa peke yake, kuna mifuko unawekeza
kwenye soko la fedha tu yaani katika benki na hati fungani mfano mfuko huu ni wa Ukwasi.
Hii ina maana kuwa mfuko huu hauna tabia ya kipande kupanda na kushuka kwa mawimbi makubwa
kwani riba, hatifungani na za mabenki huzuwa na mawimbi ya wastani ukilinganisha na mwenendo wa
faida kwenye hisa.
Watanzania ni wakati muafaka wakuchukuwa hatuwa, kuanza uwekezaji huu kwani ni mbadala wa
vibubu au kuweka fedha sehemu ambazo sarama, pia unafaida ukilinganisha na akaunti za kawaida za
akiba, changamoto zilizopo kwa vikoba.