Home Mchanganyiko Wakabiliwa na changamoto ya barabara ya kuingia hospitali ya wilaya

Wakabiliwa na changamoto ya barabara ya kuingia hospitali ya wilaya

0

**********************

Na Woinde Shizza ,Arusha 

Halmashauri ya wilaya ya ngorongoro inakabiliwa na changamoto ya barabara kuu kuu ya kuingia katika hospital ya wilaya hiyo kutopitika kwa kipindi hichi cha mvua ,ukosefu Wa uzio Wa kuzunguka hospitali hiyo  pamoja na kuchelewa kwa michango ya Mwananchi kotoka kwa ngazi za vijiji.
Hayo yamebainishwa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri ya wilaya ya ngorongoro  Peter  Lehhet wakati akisoma taarifa ya mradi Wa ujenzi Wa hospital ya wilaya ya ngorongoro  mbele ya Mwenyekiti Wa Taifa Wa wazazi CCM Taifa  alipotembekelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambapo inaongozwa na ilani ya chama cha mapinduzi.
Alisema kuwa katika jitihada za kuboresha huduma ya afya kwa  wananchi wake serikali imehakikisha kuwa halmashauri za wilaya ambazo hazikuwa na hospital za wilaya zitajenga hospital hizo ambapo kwa mwaka 2018/2019 serikali ilitenga jumla ya shilingi bilioni mia moja nukta tano (bilioni 100.5) ambayo imeelekezwa kwenye ujenzi Wa majengo Wa majengo saba kati yamajengo 22 yanayotegemewa kujegwa.
Alisema kuwa hospital hii itasaidia sana kwani kabla ya kujengwa wananchi Wa wilaya ngorongoro  walikuwa wanalazima  kufata huduma katika nchi jirani ya Kenya ,hivyo kukamilika kwake kutasaidi kupunguzia wananchi umbali n a garama za kugata  huduma katika nchi ya jirani.
Alisema kuwa fedha A  ujenzi Wa hospital hii umetokana  na mfumo Wa Wa force akaunti katika kutekeleza huu lengo likiwa ni kupunguza gharama za mradi na kuleta thamani ya fedha katika mradi husika .
Alisema kuwa serikali ilotoa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi Wa  hospital ambapo pia wananchi kupitia viongozi wao walihamasika na kukubaliana kuchangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa Kijiji ambapo hadi sasa jumla ya shilingi 30,589,400 zimekishwa kutolewa,aidha walipata fedha za basket kwa ajili ya ukamilishaji Wa miundo mbinu katika vituo vya kutolea huduma ya afya ikiwemo hospital ya wilaya.
Alibainisha kuwa wilaya ya ngorongoro imejipangakukabiliana na changamoto ambapo kupitia Tarura kujenga daraja ambapo alibainisha kuwa tayari usanifu umekwisha fanyika na utekelezaji utafanyika kwa bajeti ya mwaka 2020/2021.
” halmashauri imetenga kiasi cha shilingi 20,000,000 katika bajeti ya mwaka 2020/2021 kutoka katika mapato yq ndani kwa ajili ya kujenga uzio Wa kuzunguka Hospital hii ya wilaya ,huku tukiendelea kuhamasisha michango yao ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi 30,589,400kimetolewa kati ya shilingi 138,000,000 zilizopagwa kutolewa na vijiji vyote 69vya wilaya”alisema Lehhet
Alibainisha kuwa majengo yote yapo katika hatua za mwisho za ujenziambapo alisema kuwa  hospital hiyo itakuwa na majengo ya mwanzo saba ,ambapo aliyataja ni jengo la wagonjwa Wa nje (OPD)maabara tatu ,jengo la mama na mtoto,jengo la mionzi ,jengo la stop ya dawa,jengo la kufulia pamoja na jengo la utawala
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Taifa Edmund Mndolwa  alisema aliipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kujengo hospital hiyo kwa ni ikikamilika itawasaidia wananchi kupunguza garama za usafiri pamoja na matibabu.
Aidha aliwapongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia vyema mradi huo kwa ni wameweza kutumia kiasi cha shilingi 1,553,000,000 katika ujenzi Wa hospital hiyo kwa kusimamia wenyewe ambapo wangetumia wakandarasi wangeweza kutumia zaidi ya shilingi bilioni tatu.