Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe amevunja bodi ya muungano wa vyama vya ushirika tarafa ya lupembe MVYULU na kuagiza vyombo vya usalama kuwakamata na kuwahoji viongozi wa chama hicho kuhusu ubadhilifu ,wizi wa magari na mitambo ya kiwanda cha chai Lupembe uliofanyika 2008 baada ya muwekezaji kufanyiwa vurugu na wananchama wa ushirika.
Bashe ametoa agizo katika mkutano aliofanya na wafanyakazi wa kiwanda cha Lupembe Tea kinachomilikiwa na DOOR MECHANTILLE, muwekezaji na wanachama wa MVYULU ambapo amesema maamuzi aliyotoa amejiridhisha kutoka kwenye ripoti ya tume ya uchunguzi ya wizara na iliyoundwa na mkuu wa mkoa kwamba kulikuwa na ubadhirifu mkubwa katika chama hicho.
Amesema licha ya muwekezaji kuwa na changamoto ya kuchelewesha malipo lakini uongozi wa MVYULU umekuwa ukichumia tumboni kwao kupitia kivuli cha mgogoro hatua ambayo ikamfanya kuliagiza jeshi la polisi kuwakamata viongozi tisa wa chama hicho huku mmoja ambaye ni mwenyekiti akidai kutafuta upenyo na kutoroka .
Baada ya kuvunja bodi Bashe akamwagiza mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na maafisa ushirika kuitisha uchaguzi mpya katika AMCOS zote 9 zinazounda ushirika wa MVYULU na kasha kuunda uongozi wa chama hicho ambacho kitatoa wawakilishi wa bodi ya kiwanda ambayo wanamiliki hisa 30 huku 70 zikiwa za muwekezaji .
Akitoa ufafanunuzi kuhusu mgogoro wa umiliki wa hisa waziri Bashe amesema serikali ndiyo iliyokuwa imefanya makosa kwa kuuza hisa asilimia 70 kwa muwekezaji na kuwaacha wakulima na hisa 30 na kwamba kinachiotakiwa kufanywa na wanachama ni kufatilia haki zao serikalini badala ya kumsumbua muwekezaji na kuharibu sekta ya chai
Awali wakiwasilisha taarifa kuhusu athari za mgogoro huo uliodumu zaidi ya miaka kumi Allen Mbafu kaimu meneja wa Kiwanda anasema umesababisha wizi mkubwa wa mali za kiwanda ikiwemo magari 17,vipuri na mashine huku Ulungi ambaye ni katibu wa Mvyulu akisema mgogoro huo umesababisha kushindwa kuendesha kilimo cha chain a kusababisha hekta zaidi ya miambili kuharibika.
Ujio wa naibu waziri mwenye dhamana ya kilimo kumalizxa mgogoro huo unaibua hisia kwa wazee waasisi wa chama cha ushirika cha MVYULU akiwemo Lukule Kimilivatali na Rehema Malekela ambao wanasema kukosekana kwa maelewano baina ya wabaia hao ambao ni muwekezaji na ushirika umekuwa na madhara makubwa kwa uchumi wao na kumuomba waziri kuumaliza.
Aidha kufuatia malalamiko ya limbikizo la malipo ya mauzo ya chai Bashe akahitimisha kwa kumuagiza muwekezaji ifikapo januari 30 awe amelipa madeni yote kwa wakulima na kujipanga kuboresha huduma.