wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Daudi Mkumbo akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji
kuhusu huduma zao.
wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma
zao
AFISA Msaidizi wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Mariam Mikidadi akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga Jiji Tanga wakati wa zoezi la uelimishaji
kuhusu huduma zao. Msimamizi
wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akitoa elimu ya usomaji mita kwa wananchi wa Mtaa wa Majengo Kata ya Duga wilayani ya Tanga wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwao kuhusu huduma
zao
 
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imesema kwamba wanafikiria kuingia kwenye teknolojia ya ufungaji wa mita za maji ambazo zitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na kuzituma taarifa kwenye data base ofisini kwao.
Hayo yalisemwa na Afisa Ankra wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Daudi Mkumbo wakati akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata ya Duga Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji kuhusu huduma zao.
Alisema kwani mita hizo zitakuwa zimefungwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe na watu ambao wanashughulika na usomaji wa mita watakwenda kufanya kazi nyengine hali ambayo itarahisisha usomaji wake.
“Katika miaka ijayo tunafikiria kuanzisha mpango huo wa mita hizo lakini zile ambazo tunazotazamia kuzifunga mwaka huu ni kununua na kufungwa chombo ambacho kinaweza kupelekea mita kujisoma zenyewe na hao wasomaji waende kufanya kazi nyengine”Alisema
Afisa Ankra huyo alisema kwamba anaamini uwepo wa mita hizo utaondoa changamoto kwa baadhi ya wateja ambao wanadai kwamba wasomaji hawafiki kwenye maeneo yao kusoma mita.
“Kwa sasa kuna teknolojia ambayo mtu hataweza kusoma mita ya maji kwa umbali wa mita zaidi ya mita sita inamaana ndani ya mita sita ndio mtu anaweza kusoma maana yake kila mita ya maji itakuwa imefungwa kifaa hicho cha GPS ya eneo na ile mita ilipo atakuwa anatambulika na msomaji akifika ndani ya mita sita hawezi kudanganya”Alisema
Hata hivyo alishauri wananchi wa maeneo hayo kuacha tabia ya kutokuacha mabomba wazi wakati wanasubiri maji yakiwa yamekatika kwani hiyo ndio inaweza kuwa ndio chanzo kikubwa cha kupata bili kubwa ambayo haihusiani na matumizi ya wateja.
“Kwa sababu kipindi ambacho maji yamekatika kwenye bomba linajaa upepo hivyo wakati maji yanaporudi yakiwa na msukumo ule upepe ndio ambao unatangulia kabla ya maji unaozungusha mita na hiyo ndio chanzo kikubwa”Alisema Afisa Ankra huyo.
Hata hivyo alisema kwamba kama eneo ambalo ni Duga kuna changamoto ya miuondombinu chakavu aliwashauri kufunga maji na kutokufungua bomba mpaka wahakikishe maji yanatoka ili kuepukana na bili kuwa kubwa.
“Lakini ukifungulia maji wakati hamna maji kwani utasababisha bili kubwa wakati maji yanayorudi huo ni ushauri mpaka pale ambako yataweza kurekebisha miundombuni ili maji yaweze kutoka muda wote”Alisema
Hayo yanatokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kwenye mtaa wa Majengo Kata ya Duga ambao walilamika kwamba wanapata bili kubwa wakati muda mwengine maji yanakuwa yamekatika.
Akizungumza mmoja wa wananchi hao Selemani Rashid alisema kwamba kwenye suala la usomaji wa mita wanaokwenda kufanya hivyo lazima wakutane na watu waliopo kwenye maeneo wanayokwenda.
“Lakini muweke utaratibu kwamba wasomaji wanapokwenda kusoma mita lazima wakutane na watu kwa lengo kwamba wakati wa usomaji wa mita hizo washughudie namna zinazosomwa ili kuonda dhana kwamba hawapiti kusoma maji”Alisema
Naye kwa upande wake mkazi mwengine wa mtaa huo Magreth Jeros alisema kwamba maji yanaweza kukatika asubuhi mpaka jioni hayatoki na sio siku moja hadi siku mbili lakini bili zinazokuja zinakuwa ni kubwa sana.