Kiungo Ibrahim Ajibu akiwaongoza wenzake baada ya kikosi kuwasili kisiwani Pemba jana tayari kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo inatarajiwa kuanza leo huku mabingwa hao wa Tanzania wakicheza mechi yao ya kwanza kesho kwa kumenyana na Zimamoto Saa 10:15 Uwanja wa Gombani, mchezo ambao utarushwa LIVE na Azam Sports 2
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi kesho Januari, 7,2020 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kwa ajili ya kumtafuta bingwa wa taji hilo.
Taji hilo lipo mikononi mwa Azam FC ambao tayari wameshatia timu visiwani Zanzibar.
Azam FC itarusha kete yake ya kwanza kesho dhidi ya Mlandege huku Mtibwa Sugar yeye atarusha kete yake mbele ya Chipukizi.
Michuano hiyo inajumuisha jumla ya timu nane ambapo leo Simba nao wametia timu visiwani Zanzibar.
Simba ipo kundi B litakalokuwa Pemba na litatumia Uwanja wa Gombani ikiwa na timu za Mtibwa, Chipukizi na Zimamoto kwa upande wa Azam FC ipo kundi A itatumia uwanja wa Amaani ikiwa na Yanga, Mlandege na Jamhuri.
Simba kete yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Zimamoto Januari, 7 sawa na Yanga ambayo itamenyana na Jamhuri.