Katibu Mkuu Wa Madini Prof. Simon Msanjila akichangia hoja wakati wa majadiliano |
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza jambo wakati wa majadiliano hayo |
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiongoza Kikao na wataalamu waliofanya tathmini ili kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti ili kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza matakwa ya Nchi wanachama kwa kutokuruhusu rasilimali za nchi kutumika kuchochea maasi.
……………………………………….
Na Nuru Mwasampeta, DSM
Imeelezwa kwamba Kabla ya kuisha Mwaka huu wa Fedha 2019/2020 Tanzania itakuwa imepata Cheti Maalumu kitakachoitambulisha kuwa ni nchi iliyokidhi
Vigezo vya nchi zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini yakiwemo madini kutochochea machafuko kwa nchi wanachama za maziwa makuu.
Vigezo vya nchi zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini yakiwemo madini kutochochea machafuko kwa nchi wanachama za maziwa makuu.
Cheti hicho kitaiwezesha nchi kutathmini na kutoa vibali kwa wachimbaji, wauzaji na wasafirishaji wa Madini ya Bati (tin), dhahabu na Tangsten kuuza Madini hayo nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo tarehe 18 Desemba, 2019 jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kilicholenga kupokea ripoti juu ya tathmini iliyofanywa kwa lengo la kujiridhisha
endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti cha nchi wanachama zilizokidhi matakwa hayo.
endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti cha nchi wanachama zilizokidhi matakwa hayo.
Ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Naibu Waziri Nyongo aliyeambatana na Katibu Mkuuwa Wizara hiyo Prof. Simon Msanjila na wataalamu kutoka viongozi wa
sekretariati ya Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Maziwa Makuu yenye jumla ya nchi wanachama 12 ulioundwa kwa lengo la kulinda rasilimali zinazopatikana katika nchi zao ili zisitumike katika kusababisha na
kuendeleza machafuko katika nchi wanachama.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri Stanslaus Nyongo alisema anatarajia nchi za Rwanda, Uganda na Kongo zitafanya kazi kwa pamoja ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho Mapema iwezekanavyo kutokana na nchi kukidhi matakwa muhimu ya kupewa cheti hicho.
Nyongo alisema kuwa tathmini iliyofanywa na Sekretarieti Nchini kuanzia tarehe 13 hadi 18 Desemba, 2019 imeonesha wazi namna Serikali ya Tanzania
inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike kuharakisha mchakato wa nchi kupewa cheti hicho.
inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike kuharakisha mchakato wa nchi kupewa cheti hicho.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila aliwataka wajumbe kukamilisha kazi hiyo kabla ya Mwaka kuisha ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho Mapema iwezekanavyo.
Akizungumza Namna mchakato wa tathmini hiyo ilivyofanyika, Gerard Nayuburundi mmoja kati ya wataalamu waliofanya tathmini nchini kutoka Burundi
alisema wako tayari kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo waliyoyapata ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.
alisema wako tayari kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo waliyoyapata ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.
Aliongeza kuwa, wamejiridhisha na namna Tanzania inavyolinda na kuwasaidia wawekezaji ili Uwekezaji wao nchini kuwa na m tija.
Akizungumzia namna tathmini hiyo ilivyofanyika Gerard alisema ilihusisha mahojiano na Ukaguzi wa taarifa mbalimbali wa namna mchakato wa uchimbaji, uuzaji,
na usafirishaji wa rasilimali madini unavyofuata taratibu zilizowekwa na nchi wanachama.
na usafirishaji wa rasilimali madini unavyofuata taratibu zilizowekwa na nchi wanachama.
Mpaka sasa ni nchi tatu tu za Uganda, Rwanda na Kongo zinazomiliki cheti hicho ambapo Tanzania itakuwa nchi ya nne kupewa cheti hicho muhimu.